SoC01 Upataji fursa, ajira kwa haraka kwa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii

SoC01 Upataji fursa, ajira kwa haraka kwa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
May 21, 2019
Posts
14
Reaction score
24
Namna nzuri ya kuitumia mitandao ya kijamii kupambana na soko la ajira pia kufumania fursa mbalimbali kutokana na uhitaji wako.

Vijana waliohitimu vyuo vikuu wanalalamika hakuna ajira hii makala itasaidia vijana ambao bado wako vyuo na waliomaliza pia wakulima, wafanya biashara nk.

Kwa muhitaji wa fursa ambazo zinaendana na mahitaji yake kwenye mitandao ya kijamii yazingatiwe yafuatayo.

1. Kwa Mtu ambaye anahitaji ajira kutokana fani/ utaalamu wake sasahivi sio muda wa kutuma(post) eti unakula Bata au vitu ambavyo havikupi faida yeyote Cha kufanya Ni nii...... endelea kusoma chini.

2. Kuweka fani( professional) kwenye akaunti za mitandao ya kijamii Kama unazo Facebook, instagram, Tweeter, linkedin, Jamiiforums, WhatsApp nk. Itawarahisishia watu, kampuni, taasisi kujua umebobea katika fani ipi na wanaweza kukutafuta kwa uharaka Ila Cha kuzingatia posts zako ziendane na fani yako au vitu vya kijamii.

3. Fuatilia( follow) makundi, taasisi, kampuni, wizara na watu mbalimbali ambao kada zao zinafanana na fani au kada yako na zinazoendana na kada yako ili fursa watakayo ituma kwenye kurasa zao. Ni rahisi kuziona kwa uharaka na kuchangamkia fursa hiyo yaweza kuwa ya ajira, kilimo, kujitolea, mafunzo n.k.

4. Vijana na watu wengine tupende kujitoa au kujitolea katika shughuli za kijamii, kampuni, taasisi n.k ili uoneshe una Nini na watu watajua unakitu ndo unapata fursa mbalimbali ukikaa nyumbani Nan atajua una unini Cha kufaidisha jamii, kampuni au taasisi pia uaminifu na nidhamu kwenye kazi na kwa jamii.

Mfano Kuna kijana kamaliza chuo kikuuu mwaka Jana, 2020 alikuwa akitumia mitandao kwa namna nilivyoeleza sasa hivi Ni Rais wa SOA hub Tanzania ( sustainable ocean allience) , country coordinator of WIOMSA ( West Indian ocean marine society association) pia Ni CEO wa kiwanda Cha kuchakata platiski na kutengeneza matofali na vigaee vya uwanii yote Ni kufukua fursa kwa mitandao.

Ajira zipo nyingi kila siku zinatangazwa kwenye kurasa za kampuni husika, taasisi na vikundi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom