UPDATE 1: Mfahamu "Jenerari" atakaeongoza "Jeshi" la Simba SC 01.10.2016.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Mashabiki na Wanachama wa Simba SC tukiwa tunaendelea kuzihesabu siku zilizobaki kuelekea katika "vita' yetu dhidi ya Yanga SC.. namleta kwenu Jenerari atakaetuongoza siku hiyo.

Huyu Jenenari nani?
Ni Joseph Marius Omog, ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba SC. Omog ambaye ana heshima kubwa sana barani Africa, alizaliwa miaka 44 nchini Kameruni.

Omog ana uzoefu gani katika soka?
Ni ngumu sana kumtenganisha Omog na mpira, kwani tangu akiwa kinda amepiga mpira mwingi sana nchini kwao. Mojawapo ya timu aliyocheza kwa kiwango kikubwa ni Dragon Yaounde. Hakudumu sana dimbani, kabla hajachukua maamuzi magumu ya kusomea ukocha.

Ni "magamba" gani ya ukocha aliyo nayo katika kabati lake?
Ukiuliza wachambuzi wa soka nchini Kameruni, Omog ni nani? Jibu lao hua ni.. "Omog is highly learned man in formal coaching training"
Baadhi ya "magamba" aliyonayo ni;
1. Amesoma Sports and Physical Education ya katika chuo bora cha soka Africa, kiitwacho Higher Institute of Youth and Sport, kilichopo nchini Kameruni.
2. Ana UEFA license level B, aliyoipata "kwa waojua" nchini Ujerumani mnamo mwaka 1987.

Ni timu gani alizowahi kufundisha?
2001 - 2010... Timu ya Taifa ya Kameruni
2011 - 2013... AC Leopards ya Congo Brazaville
2013 - 2014... Azam FC
2016 - ............ Simba SC

Je kuna mafanikio yoyote aliyowahi kupata kama kocha?
Baadhi ya mafanikio yake ni;
2011 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa FA Cup ya nchini Congo.
2012 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa makombe mawili, ambayo ni CAF Confederation Cup na Congo Premier League.
2013 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa Congo Premier League.
2014 - Aliiongoza Azam FC kutwaa taji lake la kwanza la ligi kuu.
NOTE:
Mwaka 2012 Joseph Marius Omog alikamata namba 2 katika tuzo ya kocha bora barani Africa, nyuma ya Renard Herve.

Huyo ndo Joseph Marius Omog, Jenerari ambae anaenda kuongoza Mashabiki na Wanachama wa Simba SC duniani katika katika "vita" hiyo.. Naimani tunaenda kushinda asubuhi sana.

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING.
Neno langu kwa Masau Bwire.. "kilichowakosa JKT Ruvu siku ya jumamosi.. ndicho mtakipata leo.".

cc Makoye Matale na "wenzake".
 
Hahaha we jamaa unatia huruma kweli,sisi hua hatunaga mpira wa mdomoni,ngoja leo unyooshwe kwanza na ruvu.
 
Haha.. kwani Mkuu kuna kitu nimeongea cha uongo hapo?

Narudia tena; "kilichomkosa JKT Ruvu, kitampata nduguye Ruvu Shooting'
 
Kwa hiyo kuanzia 2001 hadi 2010 Omog alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Cameroon,

1.Je alikuwa anafundisha timu ya wanawake au ile Indomitable Lions ya kina Etoo,Olembe,Njitap,Ndief,Makoun,Kameni ?
 
Kwa hiyo kuanzia 2001 hadi 2010 Omog alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Cameroon,alikuwa anafundisha timu ya wanawake au ile ya kina Etoo,Olembe,Njitap,Makoun,Kameni ?

Hiyo hiyo ya akina Etoo.. Na alianza kama kocha msaidizi mwa 2001 kabla ya kupandishwa na kua kocha Mkuu mwaka 2003.
 
So 2003 hadi 2010 Omog alikuwa kocha mkuu wa Indomitable Lions ?
Endelea kuwadanganya wamchangani wenzako,labda alifundisha timu ya wanawake
 
Simba Vs Ruvu Shooting
Uhuru, Dar es salaam 07/09/2016

Ruvu Shooting (Line Up)

1. Abdallah Rashid Abdallah 30
2. Damas Julius Makwaya 20
3. Mau Alli Bofu 23
4. Frank Faraja Msese 16
5. Shaibu Athuman Nayopa 26
6. Jabir Aziz Stima 25
7. Abdulhaman Musa Abdulhaman 17
8. Shabani Abdallah Kisiga 10
9. Said Abas Dilunga 3
10. Fully Zulu Maganga 28
11. Claide Loita Wigenge 13

Sub
Gk Bidii Abdallah Hussein 18
Said Iman Madega 19
Yusuph Innocent Nguya 2
Baraka Mtuwi 15
Raphael Bathromayo Keyala 8
Issa Said Kandulu 11
Renatus Pastory Kisese 5
 
Jeshi la Simba dhidi ya Ruvu shooting
Vicent Angban (22)
Malika ndeule (3)
Mohamed Hussein (15)
Novaty lufunga (21)
Method mwanjali (17)
Jonas mkude (20)
Shiza kichuya (25)
Said ndemla (13)
Laudit mavugo (11)
Ibrahim ajib (23)
Kazimoto( 8)

Akiba
Peter manyika(18)
Abdi banda(24)
Emmanuel simwanza (5)
Mohamed Ibrahim (4)
Jamal mnyate (14)
Mzamiru yassin(19)
Fredrick Blagnon (27)
 
Angalia makocha wa Indomitable Lions
uploadfromtaptalk1473247522123.png
 
So 2003 hadi 2010 Omog alikuwa kocha mkuu wa Indomitable Lions ?
Endelea kuwadanganya wamchangani wenzako,labda alifundisha timu ya wanawake

Mkuu hebu pitia hapa, kuna kitu unaweza kujifunza

"Mwaka 2001 aliteuliwa kuwa Msaidizi wa kocha Mjerumani, Winfried Schafer katika timu ya taifa ya Cameroon, Simba Wasiofungika chini ya Nahodha Samuel Eto’o haswa kutokana na kujua kwake Kijerumani, kwa sababu kocha huyo alikuwa hazungumzi Kiingereza wala Kifaransa, lugha zinazotumika nchini humo.
Mwaka 2003 aliteuliwa kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa baada kuondoka kwa Winfried Schafer, lakini akafukuzwa mwaka 2010 kutokana na matokeo mabaya na kushindwa kuiwezesha Cameroon kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika."

Source; Simba yampa ukocha Joseph Omog - Bongosoka

Lugha inanipiga chenga, naomba unitafsirie aya ifuatayo ambayo imeandikwa na Wakameruni wenyewe.

"In 2003 he was appointed head coach of the Indomitable Lions after the departure of Winfried Schafer but was dismissed in 2010 for lack of results after he failed to qualify Cameroon for the African nation's championship"

Source: Profile - Marius Omog, Flag Bearer of Cameroonian Coaches
 
Wamchangani acha kujidhalilisha kwa kuokoteza story ambazo zinakuletea hata shida kuzielezea,tafuta reliable source. Hiyo story inasema kuwa Omog alifundisha Indomitable Lions kuanzia 2003-2010 (hii hata Hans Pope lazima atakubishia).Makocha waliofundisha Cameroon na miaka waliofundisha nimeiweka hapo juu.Miaka ya 2004,2006,2008 kulikuwa na michuano ya CAN na Cameroon haikufundishwa na Omog
 
Mkuu hebu pitia hapa, kuna kitu unaweza kujifunza

"Mwaka 2001 aliteuliwa kuwa Msaidizi wa kocha Mjerumani, Winfried Schafer katika timu ya taifa ya Cameroon, Simba Wasiofungika chini ya Nahodha Samuel Eto’o haswa kutokana na kujua kwake Kijerumani, kwa sababu kocha huyo alikuwa hazungumzi Kiingereza wala Kifaransa, lugha zinazotumika nchini humo.
Mwaka 2003 aliteuliwa kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa baada kuondoka kwa Winfried Schafer, lakini akafukuzwa mwaka 2010 kutokana na matokeo mabaya na kushindwa kuiwezesha Cameroon kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika."

Source; Simba yampa ukocha Joseph Omog - Bongosoka

Lugha inanipiga chenga, naomba unitafsirie aya ifuatayo ambayo imeandikwa na Wakameruni wenyewe.

"In 2003 he was appointed head coach of the Indomitable Lions after the departure of Winfried Schafer but was dismissed in 2010 for lack of results after he failed to qualify Cameroon for the African nation's championship"

Source: Profile - Marius Omog, Flag Bearer of Cameroonian Coaches
Labda Cameroon ya Mwananyamala
 
Mashabiki na Wanachama wa Simba SC tukiwa tunaendelea kuzihesabu siku zilizobaki kuelekea katika "vita' yetu dhidi ya Yanga SC.. namleta kwenu Jenerari atakaetuongoza siku hiyo.

Huyu Jenenari nani?
Ni Joseph Marius Omog, ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba SC. Omog ambaye ana heshima kubwa sana barani Africa, alizaliwa miaka 44 nchini Kameruni.

Omog ana uzoefu gani katika soka?
Ni ngumu sana kumtenganisha Omog na mpira, kwani tangu akiwa kinda amepiga mpira mwingi sana nchini kwao. Mojawapo ya timu aliyocheza kwa kiwango kikubwa ni Dragon Yaounde. Hakudumu sana dimbani, kabla hajachukua maamuzi magumu ya kusomea ukocha.

Ni "magamba" gani ya ukocha aliyo nayo katika kabati lake?
Ukiuliza wachambuzi wa soka nchini Kameruni, Omog ni nani? Jibu lao hua ni.. "Omog is highly learned man in formal coaching training"
Baadhi ya "magamba" aliyonayo ni;
1. Amesoma Sports and Physical Education ya katika chuo bora cha soka Africa, kiitwacho Higher Institute of Youth and Sport, kilichopo nchini Kameruni.
2. Ana UEFA license level B, aliyoipata "kwa waojua" nchini Ujerumani mnamo mwaka 1987.

Ni timu gani alizowahi kufundisha?
2001 - 2010... Timu ya Taifa ya Kameruni
2011 - 2013... AC Leopards ya Congo Brazaville
2013 - 2014... Azam FC
2016 - ............ Simba SC

Je kuna mafanikio yoyote aliyowahi kupata kama kocha?
Baadhi ya mafanikio yake ni;
2011 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa FA Cup ya nchini Congo.
2012 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa makombe mawili, ambayo ni CAF Confederation Cup na Congo Premier League.
2013 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa Congo Premier League.
2014 - Aliiongoza Azam FC kutwaa taji lake la kwanza la ligi kuu.
NOTE:
Mwaka 2012 Joseph Marius Omog alikamata namba 2 katika tuzo ya kocha bora barani Africa, nyuma ya Renard Herve.

Huyo ndo Joseph Marius Omog, Jenerari ambae anaenda kuongoza Mashabiki na Wanachama wa Simba SC duniani katika katika "vita" hiyo.. Naimani tunaenda kushinda asubuhi sana.

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING.
Neno langu kwa Masau Bwire.. "kilichowakosa JKT Ruvu siku ya jumamosi.. ndicho mtakipata leo.".

cc Makoye Matale na "wenzake".
Pale Azam aliwezeshwa sana lakini matokeo hayakulingana na investments. Tusubiri. Badala ya Omgo atakuwa Omoro
 
Kwa hiyo kuanzia 2001 hadi 2010 Omog alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Cameroon,

1.Je alikuwa anafundisha timu ya wanawake au ile Indomitable Lions ya kina Etoo,Olembe,Njitap,Ndief,Makoun,Kameni ?
Jamaa ni muongo kweli kweli yanim
 
Sembo rekodi hizo zipo ulaya kocha anafundisha miaka 15 huku kwa waswahili figisu figisu nyingi ni ngumu sana.Na hiyo kwa Africa anayo mzee hassan shehata wa Egypt na sio kufundisha tu na ndoo alichukua mara 3 mfululizo.
 
Back
Top Bottom