Update: Biashara ya mbao kutoka Njombe kwenda mikoa mingine kama Dar es Salaam na Dodoma

Update: Biashara ya mbao kutoka Njombe kwenda mikoa mingine kama Dar es Salaam na Dodoma

What if umekadiriwa kwa mwaka lakini hujaenda hata mara moja kuchukua mzigo???? Tumia akili kijana wa TEC hoja zako ni nyepesi sana kuepuka double taxation maana yake hapo makadirio kwa mwaka yamekufa automatically lakini hata yangekuepo ni rahisi kwa TRA kujua na kukadiria kwa sababu ile turnover itaonesha ukubwa au udogo wa biashara yako!
Binti TEC wanakuumiza sana
 
***** huo msururu wa kodi na ushuru na hapo bado VAT au sijui income tax, ***** nimeamini chanzo cha umaskini ni kuongozwa na wajinga, hapo no chance utaweza kukuza mtaji au kuajiri na kulipa vizuri
 
Kwa wale wafanyabiashara mnaokuja kujumua mbao wilaya ya Njombe ningependa kuwataarifu juu ya mabadiliko ya ushuru na kodi ya TRA

•Kwasasa wilaya ya njombe wanacharge 3% ya thamani ya mbao zote ulizopakia kwenye gari kama ushuru tofauti na zamani walivokuwa wanacharge 100Tsh kwa ubao.

•TRA kwasasa wanacharge 2% ya thamani ya mbao zote ulizopakia kwenye gari tofauti na zamani walivokuwa wanataka risiti ya manunuzi ambayo ulikuwa unaipata kwa 300,000Tsh.

NB: Wilaya ya njombe bado wanacharge ushuru wa magogo kwenye kila bidhaa ya msitu utakayosafirisha.

Kila geti la ukaguzi utakalikuwa unapita lilipo ndani ya wilaya ya Njombe utalipia 15,000/= kama ushuru wa magogo

KABLA HUJAJA WILAYA YA NJOMBE KUNUNUA MBAO ZINGATIA GHARAMA ZIFUATAZO ILI USIPATE HASARA

•Manunuzi

•Upakiaji: 150,000/=

•Usafiri:

•Ushuru: 3% ya thamani ya manunuzi ya mbao

•TRA: 2% ya thamani ya manunuzi ya mbao

•Transit pass: 15,000/=

•Ushuru wa Transit pass: 20% ya gharama ya Transit pass

•Barua ya serikali ya mtaa: 5,000/=

•Ushuru wa magogo: 50,000/= hadi 150,000/= itategemea umenunua eneo gani na utapita mageti mangapi

•Kuhakiki uzito mizani: 15,000/=

NB: Hakikisha unakuwa na cash ya akiba ikitokea uzito umezidi wakati unahakiki mizani unatakiwa kulipa vijana wapunguze mzigo.


KUMBUKA KUWA NA NYARAKA ZIFUTAZO KABLA YA KUANZA SAFARI ILI USISUMBULIWE NJIANI

•Kibali cha kufanya biashara ya mbao (Certificate of registration of forest produce dealer or trader)

•Transit pass

•Barua ya serikali ya mtaa mahali uliponunua mbao

•Risiti ya ushuru wa mbao

•Risiti ya ushuru wa magogo

•Risiti ya malipo ya 20% ya transit pass

•Hakikisha gari uliyokodisha ina tembea na risiti ya mauzo ya huduma

MUHIMU: Wakati wa kukata transit pass na ushuru usidanganye kiasi cha mbao ulizonunua hii ikigundulika njiani itakusababishia kupigwa faini si chini ya 500,000Tsh

Hakikisha eneo lillilojazwa kwenye transit pass linaendana na eneo kibali cha kufanya biashara ya mbao kimeandikishwa

La mwisho hakikisha taarifa muhimu kama namba za gari,majina ya dereva nk vinajazwa kwa usahihi wakati wa kukata transit pass

KAMA UNAHITAJI MBAO KUTOKA WILAYA YA NJOMBE HIZI NDO BEI ZAKE KWA SASA

2by4. 3400
2by6.4500
2by2.1200
1by8.4500
1by6 2800
1by4. 1200
1by10 9800

View attachment 3537114View attachment 3537114View attachment 3537114

MAWASILIANO
0748874928
(Piga/sms/whatsapp)
Nije na mtaji kiasi gani niweze kutoa mzigo huko kwenda dar?
 
Nije na mtaji kiasi gani niweze kutoa mzigo huko kwenda dar?
•Siwezi kusema kiasi cha moja kwa moja mpaka nijue size za mbao unazohitaji maama size za mbao zinaamua gharama za manunuzi.

•Lakini kwa jicho la uzoefu andaa 14M minimum.
 
***** huo msururu wa kodi na ushuru na hapo bado VAT au sijui income tax, ***** nimeamini chanzo cha umaskini ni kuongozwa na wajinga, hapo no chance utaweza kukuza mtaji au kuajiri na kulipa vizuri
Bei za sokoni zimezingatia hivo vitu piga hesabu zako vizuri utapata faida.
 
•Siwezi kusema kiasi cha moja kwa moja mpaka nijue size za mbao unazohitaji maama size za mbao zinaamua gharama za manunuzi.

•Lakini kwa jicho la uzoefu andaa 14M minimum.
Hapo huja jumuisha gharama za usafiri wa mzigo mf. Kutoa Njombe - Dar ?
 
Back
Top Bottom