Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Hatima ya dhamana ya Boniface Jacob "Boni Yai," itajulikana leo, Septemba 23, 2024, wakati Mahakama itakapotoa uamuzi kuhusu maombi ya Serikali ya kuzuia dhamana yake. Boni Yai alikamatwa na kuletwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambapo alikabiliwa na mashitaka mawili, ambayo aliyakana.
Upande wa mashitaka, ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, ulieleza kwamba upelelezi bado haujakamilika na kuwasilisha maombi mawili: moja ikihusisha kuingiliwa kwa vifaa vya kielektroniki vya mshitakiwa na nyingine ikidai kuzuia dhamana kwa ajili ya usalama wa mshitakiwa.
Katuga alidai Yai alieleza kuwa anajua atatekwa na kuuawa. Hata hivyo, mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Peter Kibatala, walipinga maombi hayo wakidai kuwa yalifanywa kinyume cha sheria na yana kasoro.
UPDATE
Uamuzi wa dhamana ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob 'Boni Yai' umekwama kutokana na Jeshi la Magereza kushindwa kumfikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kilichoelezwa mahakamani hapo kuwa hakuna usafiri wa kumfikisha mahakamani hapo.
Mahakama hiyo itatoa uamuzi tarehe 26 Septemba 2024, siku ya
---
Pia soma