UPDATE: Leah Ulaya arejeshewa Urais wa CWT

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais wa CWT aliyesimamishwa, Leah Ulaya amefika mbele ya wajumbe wa mkutano Mkuu kwa ajili ya kutoa utetezi wake wa kwa nini arudishwe katika nafasi yake.

Ulaya ameingia ukumbini kwa kelele za wajumbe walipoimba wimbo wa mlete mzungu na wimbo wa mshikamano.

Dakika chache kabla ya kuingia kwa Ulaya kutoa utetezi wake, ilitokea vurugu kubwa ndani ya ukumbi hata wajumbe wakaamua kumtoa kwa kumzonga na kumsukuma nje.

Mara baada ya kutolewa, wajumbe walimchagua mjumbe kuongoza kikao ambapo Kaimu Katibu alirudi ukumbini na kuwataka wajumbe watulie ili kikao kiendelee.

Tuhuma za Rais hiyo zilizimwa na Kaimu Katibu mbele yake na wajumbe kisha akapewa nafasi ya kujitetea ambapo alitumia dakika 14 kutoa utetezi mbele ya wajumbe huku akiomba kurejeshwa katika nafasi yake kwamba aliondokewa kwa maonezi.

Wajumbe hawakuwa na swali la kumuuliza ndipo akaelezwa kutoka nje na wajumbe wakahojiwa wengi wakasema arudishwe huku sauti chache zikisema asirudishwe na Mwenyekiti akasema waliosema arudishwe wameshinda.

Ulaya arudishwa

Saa 6.00 Ulaya aliitwa ukumbini akisindikizwa na kundi la wajumbe waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu wakitaka akalie kiti.

Akitoa neno la shukrani mbele ya wajumbe amesema bado ana nguvu ya kuwatumikia walimu na kwa namna yoyote atabaki ndani ya ukumbi kuendesha mkutano.

"Nimekaa nje kwa mwaka mmoja na nusu, nipeni nafasi niwatumikie, naahidi kuvunja makundi na kutanguliza maslahi ya walimu mbele, sina kinyongo na mtu yeyote zaidi ya kuchapa kazi," amesema Ulaya.

Amewaomba viongozi waliostaafu akiwemo Gratias Mukoba na Ezekiel Uluoch kusema neno, na waliposimama walimtaka kuchapa kazi kwa nguvu kwa maslahi ya walimu wote.

MWANANCHI
 
Mpe Hongera sana na mwambie kwamba anasalimiwa na JKT mate wake Bulombora Operation Vyama Vingi. Yeye alikuja Bulombora baada ya kupigwa bogi kutokea Msange JKT Tabora
 
Walimu ndio nguzo kuu ya taifa lolote; hakuna mtu atajisifu amefikia alipo bila mchango wa mwalimu. Big up walimu!
 
Daaah tuna safari ndefu sana ktk kuweka mambo ktk unyoofu, pesa mbaya sana.....

Ngoja tuone mwisho wa hii movie

Na yule Seif anaendeaje huko?
 
Back
Top Bottom