UPDATE: Mtoto aliyechomwa moto na kulazimishwa kula kinyesi chake akatwa mkono

UPDATE: Mtoto aliyechomwa moto na kulazimishwa kula kinyesi chake akatwa mkono

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
November 13, 2012

jeraha-472x300.jpg

Kushoto ni mtoto huyo akiwa amekatwa mkono wa kushoto ambao uliunguzwa vibaya na mama yake mdogo, kama ambavyo inaonekana katika picha ya kulia iliyopigwa jana.

Mtoto Anneth, ambaye alichomwa moto kwenye mkono na kisha kulazimishwa kula kinyesi chake na mama yake mdogo, amekatwa mkono mmoja uliokuwa umeunguzwa baada ya kubainika kuwa usingeweza kupona tena.
 
mmmh! jamani pole sana sana mtoto Aneth, Eeee Mungu wangu, huyu mtoto anaiuma sana manake she is me uwiiiiiiiii, yaani kaja uukosa mkono kwa uchomwa moto??? sijui adhabu anayostahili huyo mama kiukweli.

kwahuyu mtoto kwann madaktari wamekimbilia kumkata mkono?? it was possible kwa huu mkono kutengemaa endapo wangechukua uamuzi wa kumpeleka MOI naamin hayo manake nilishawah kushuhudia mtu alokuwa akatwe mguu Dodoma, akaomba aletwe MOI akapona kabisa.... kuondo akiungo cha mgonjwa jamani ni hatua ya juu sana, istoshe nyama za mwili huwa zinaota anyway inawezekana tu nimeongea kama layman bila basic principles mnisamehe.
 
Inasikitisha sana. Ingekua Somalia na yeye angechomwa mpaka T*go!
 
Nilikuwa nimemuoimba sana mungu kuhusu huyu mtoto nilijikuta kwenye kilio jana usiku baada ya mume wangu kunuimbia mkono wake umekatwa nilijikuta nikilia na watoto wakaanza kulia maana nilipofika niliwaonyesha zile picha za alivyoungua nikawasihi wamwombee sana mtoto mwenzao du.ila nafikiri ni kwasababu alikaa muda mrefu bila first aid my good god do something for her,
 
Hivi fukuto la hasira kwa mtoto huyu litaisha kweli??
Huyu mm anasahau kua huyu mtoto anakuwa na yeye anazeeka na nguvu kuisha?! Atakwepa lipizo la hasira kweli?
Tumwachie Mungu, yeya ahukumuye kwa haki. Naumia sana
 
Hii story haikamilishwi. Baba na mama wa mtoto wako wapi? Na huyo maaluni yuko wapi?
Nafikiria mama zetu wadogo wanavyotupenda na kututreat like kids! Ni muhimu kufundisha watoto kupendana ili hata wakiwa wakubwa cha mwenzio ukione chako.
 
Huyo mama yake mdogo alichukuliwa hatua gani za kisheria?
 
nimelia kwa kweli. Mungu tusaidie tulee watoto wetu na watoto wa wengine kwa upendo ulio sawa. Mungu wangu tupe maisha marefu tulee watoto wetu mpk wawe wakubwa wenye kujielewa kabla ya kutuchukua na kuwaacha wakutane na mama wadogo walioonyesha upendo mkubwa wakati uko nao. Kumbe ni chui waliovaa ngozi na roho ya Mbuzi.
 
Huyu mama ni wa kuchoma,jamani katoto kazuri Ee Mungu nijalie uhai tu nilee mwanangu mwenyewe hata kama hatuna chakula hvyo hvyo,uwii kweli kuna wanawake wabaya hivi?jamani Mungu amuadhibu hapa hapa tukiona,
 
Dah!Kama Haupo kizazi chako kinaangamia kama utani!huyo mama mdogo ni wakuua Kabisa
 
naona hipo haja kwa serikali za mitaa kuwa wanachukua hatua mapema, kwa masuala ya watoto kudhulumiwa haki zao, sio kusubiri kama hivi matokeo yake ni kidonda cha kudumu. inasikitisha lakini wizara husika nazo ziko kisemina semina zaidi ya kuwa in the grass root.
 
jamani nimeiona dunia kwa namna ya ajabu siku ya leo, hivi kweli mungu atasamehe hata haya???
Mungu ampe faraja mtto Aneth, mkono haupo ila ulobaki waweza kufanya makubwa maishani mwake, Mungu ni mwema sana, hatampa jaribu kama hili kisha kukosesha mlango wa kutokea. nakutakia upone haraka ma name na Mungu akukuze uje uwe mtu bora kwa taifa hili.

wazazi wenzangu tukeshe kusali ili Mungu awawekee watoto ulinzi wake mwenyewe. Pia jamani hatujui wazazi wa huyu mtt walipo ila nafkir ni bora kila mzazi alee manae mwenyewe kuliko kutegemea ndugu uwapo na uhai.
 
Tatizo ni kwamba jamii pia hushuhudia hay mambo nakunyamaza majirani waliona jinsi huyu dada anavyomyanyasa huyu mtoto mpaka imefikia kumchoma ndio wanajitokeza.

Kuna mtoto mmoja alikuwa anakaa na shangazi yake alikuwa anamyanyasa sana sana kila ikifika saa mbili usiku ni kipigo na kutumwa dukani,bahati house gal wangu akaja niambia, nikamwita yule mtoto akaniambia ni kweli naanataka kurudi kwao ahaaa kale katoto kajanja kalikariri namba ya dada yaje nijawapigia kwao nikawaeleza mkasa kesho yake ya asubuhi yake mtu japanda gari kutoka singida akaondoka walinishukuru sana.

Hivi ndivo inavotakiwa mnaona mtoto anateseka watu kimya leo hii majirani wanalia lia tu hapo shame on them
 
mbona hakuwa ameungua kiasi cha kukatwa mkono?lawama ni kwa serikali kukosa madawa ya kisasa na vifaa vya kisasa bado 2na2mia technology ya mwaka 47 pole sana mtoto.du matunda ya miaka 50 ya uhuru.
 
Hili la mama mdogo haliniingia hata kidogo!

Hivi mpaka sasa huyo mama yupo uraiani jamani?
 
Mimi hizi habari huwa zinaniumiza hadi machozi jamani
Eee Mwenyezi Mungu, nakumba utujalie wakina mama wote uhai, nguvu, upendo na uwezo wa kuwalea watoto wao hadi wakue - Amina
 
Back
Top Bottom