Tatu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2006
- 1,143
- 372
Kama kichwa cha Habari kinavyosema, zaidi ya wiki sasa imepita toka nilete hii changamoto iliyopo katika lugha yetu ya Kiswahili.
www.jamiiforums.com
Nashukuru kwa wale wote waliochangia na pia imedhihirisha wazi kwamba changamoto hii ipo.
Kwa muda sasa binafsi nimekuwa nikifanyia kazi changamoto hii. Nilifikiria namna ya kuwezesha jamii kushiriki kutoa mawazo yao katika kutafsiri maneno ya Kingereza ambayo hayana tafsiri rasmi ya Kiswahili.
Nilifikiria njia mbalimbali za kutatua hii changamoto. Mwisho wa siku, technology imekuwa ndio jibu sahihi na rafiki ambayo inaweza kutatua hii changamoto. Kwa jinsi mabadiliko na matumizi ya Tehama yanavyoongezeka, nafikiri njia hii itakuwa rahisi zaidi kufikia jamii kubwa.
Kwa maana hiyo, nimetengeneza application ya simu ya mkononi ambayo unaweza kupakua kutoka Google Play Store. Ni dhahiri kwamba application hii ni kwa wale wanaotumia simu za Android pekee. Jinsi mwitikio utakavyokua, watumiaji wa iOS itabidi wasubiri kwa sasa.
Application inapatikana katika link hapa chini.
play.google.com
Bahati nzuri pia, wiki iliyopita nimesikia kwenye taarifa ya habari kwamba Tanzania na Kenya wameweza kufanikisha muswada wao Umoja wa Mataifa, UN, wa kutambua July 7, kuwa siku ya Kiswahili duniani kote. Pia, habari hiyo imesema Kiswahili kinatumika katika nchi zaidi ya 100 duniani.
Kwa maana hiyo tuna kazi ya kufanya.
Naomba neno moja tu la Kingereza ambalo halina tafsiri rasmi ya Kiswahili
Mkuu yapo, tena ni mengi tu, mathalani yafuatayo, 1. Achilles heel 2. Mutatis mutandis 3. Ceteris paribus 4. Dsyfunction 5. other technical jargon 6. n.k, n.k Orodha nzuri. Tuna kazi ya kufanya....
Nashukuru kwa wale wote waliochangia na pia imedhihirisha wazi kwamba changamoto hii ipo.
Kwa muda sasa binafsi nimekuwa nikifanyia kazi changamoto hii. Nilifikiria namna ya kuwezesha jamii kushiriki kutoa mawazo yao katika kutafsiri maneno ya Kingereza ambayo hayana tafsiri rasmi ya Kiswahili.
Nilifikiria njia mbalimbali za kutatua hii changamoto. Mwisho wa siku, technology imekuwa ndio jibu sahihi na rafiki ambayo inaweza kutatua hii changamoto. Kwa jinsi mabadiliko na matumizi ya Tehama yanavyoongezeka, nafikiri njia hii itakuwa rahisi zaidi kufikia jamii kubwa.
Kwa maana hiyo, nimetengeneza application ya simu ya mkononi ambayo unaweza kupakua kutoka Google Play Store. Ni dhahiri kwamba application hii ni kwa wale wanaotumia simu za Android pekee. Jinsi mwitikio utakavyokua, watumiaji wa iOS itabidi wasubiri kwa sasa.
Application inapatikana katika link hapa chini.
KuKi - Apps on Google Play
Elevate Kiswahili! Collaborative Effort to Translate English into Kiswahili.