Updates: Kukamatwa kwa Wanachama wa CHADEMA Kanisani Mwanza

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Wakuu, nimepata hii updates ila kwa kweli hata kama Polisi wetu wanatumwa basi at least watumie hata akili. Why wanalazimisha kujenga chuki isiyomithilika kwenye jamii?? Was it necessary?

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi na baadhi ya Askari Wanyama pori wanaozea gerezani kwa kufanya mauwaji Kanisani. anyways wacha niwape updates

Updates

Makamanda, habari za muda huu. Mpaka sasa hivi tunaendelea kushughulikia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama walipokuwa kwenye misa jana Kawekamo.

Walioko lock up ni Katibu wa kanda ya Victoria, Mwenyekiti wa Ilemela, Katibu wa Nyamagana na wanachama wengine jumla yao ni 20.

Baada ya kumuona OCD asubuhi ya leo, alitwambia kuwa wanatuhumiwa kwa kufanya vurugu kanisani na kwamba alipigiwa simu na viongozi wa kanisa.

Ilibidi tukauone uongozi wa kanisa Katoliki jimbo la Mwanza, tumeonana na msaidizi wa baba Askofu na akatuwezesha kuongea na askofu Mkuu Renatus Kwande.

Askofu Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya Wana Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula.

Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema.

Awali asubuhi, walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani.

Baba askofu katupa msaidizi wake tukaenda naye Kirumba na ameongea na OCD, sasa ocd kageuza kwa si kanisa lilimpigia simu bali ni waumini wawili mmojawapo anaitwa Gerlad Joseph. Msaidizi wa Askofu kawasiliana naye na sasa Askofu amemtuma katibu wake Padre Nyanda, tunaendelea kumsubiri hapa kirumba.

Msimamo wetu ni:
1. Wawaachie wote bila masharti ya dhamana.

2. Au baba Askofu akawadhamini waumini wake.

Wanzagi
 
Miongoni mwao kuna Wazee wa miaka 69, 70, 75

Siamini kama Jeshi la Polisi linakosa weledi kiasi hiki! Yaani ni kweli hakuna Polisi hata mmoja mwenye akili timamu za kufanya maamuzi sahihi?

Jeshi letu halina Washauri? Hakuna Wazee? Hakuna systems? Hawana miongozo? Wao wanachojua ni kukamata tu! Kweli?
 
Duuh!

Wanatuhumiwa kufanya vurugu kanisani [emoji849][emoji849][emoji849]

Hata mtoto mchanga atastaajabu hili!!!
 
Jeshi la Polisi Tanzania waache kutumiwa na CCM , hawaoni wenzao huko Zambia vyombo vyao vya dola vya ulinzi na usalama vilikataa kutumika vibaya na chama tawala kilichongolewa tarehe 12 August 2021.
 
Yaani at least wangetumia akili kidoogo. Ukute walivyosikia Jamaa wamekaribishwa msosi wakatamani wakagonge msosi wenyewe, wakiwazia Mbuzi Katoliki na Wine wakaona no way
 
Miongoni mwao kuna Wazee wa miaka 69, 70, 75

Siamini kama Jeshi la Polisi linakosa weledi kiasi hiki! Yaani ni kweli hakuna Polisi hata mmoja mwenye akili timamu za kufanya maamuzi sahihi?

Jeshi letu halina Washauri? Hakuna Wazee? Hakuna systems? Hawana miongozo? Wao wanachojua ni kukamata tu! Kweli?

Mkuu mbona unajiuliza maswali magumu hivyo, utadhani Jeshi letu limetoka Pluto? Wakati ndio watu wale wale waliokuwepo Mwangosi akipoteza maisha n.k n.k
 
Jeshi la Polisi Tanzania waache kutumiwa na CCM , hawaoni wenzao huko Zambia vyombo vyao vya dola vya ulinzi na usalama vilikataa kutumika vibaya na chama tawala kilichongolewa tarehe 12 August 2021.
Mkuu hivi ni confirmed Mzee Lungu Chali!!?
 
Bado umeandika kiharakati zaidi.
Walenda kanisani wamevaa sare?
Ni dhambi? Wenye Kanisa wamewaombea, wamewakaribisha chakula, wewe unasema wamefanya vurugu! Wamegombea chakula? Hizo harakati ziko wapi hapo?
 
Back
Top Bottom