Updates: Kukamatwa kwa Wanachama wa CHADEMA Kanisani Mwanza

Updates: Kukamatwa kwa Wanachama wa CHADEMA Kanisani Mwanza

Kwanini wasifute mfumo wa vyama vingi, kuliko kuwadanganya Wafadhili na Wahisani wa Magharibi kuwa kuna Demokrasia, kumbe ni hadaa ili waendelee kujaziwa bakuli lao kwa njia ya utapeli wa kimataifa.

Shame on them!
 
Hizi mambo za kijinga hivi ndio huwa zinapelekea kuwepo kwa waasi.

Ccm inajinadi imefanya mambo mengi kwanini viongozi wake hawajiamini namna hiyo. Hovyo kabisa
 
Tuleteeni video za hayo mahojiano ya POLICE na ya OCD ili na sisi tujue pa kusimama na watanzania wenzetu

Kwa maneno haya matupu ni ngumu kuamini sababu CHADEMA NI KIWANDA CHA KUTENGENEZA UONGO
 
Ahsante Mungu kwa kuniepusha na kazi ya upolisi. Awali nilivyomaliza kidato Cha SITA sikuhitaji hata kwenda chuo. nilikuwa napenda sana hii kazi. Lakini kwa kuwa Mungu hakutaka niikose mbingu, ameuzuia mguu wangu usipige hatua kuelekea kwenye kazi iliyogubikwa na dhambi za Kila namna na Kila aina ya laana, ubugabire na kutokutumia akili zaidi ya kutumwa tumwa 24/7 kufanya ufala
 
Ukiingia kwenye upande wa kuonea watu hua hakuna mwisho

Ni kama kula nyama ya mwanadamu

Leo kaanza na Chadema,shika kidogo peleka kituoni,hapa na pale

Inakuja kuvunja miguu,hapa na pale

Inakuja kuua.....

Baada ya hapo Chadema,atafata NGOs,wanaharakati,wana CCM wenzake,mawaziri wenzake,etc

Baada ya hapo ataenda nchi jirani kutafuta vita,hapo ndio anashikwa anachinjwa yeye
Mungu atuepeushie hili
 
Ahsante Mungu kwa kuniepusha na kazi ya upolisi. Awali nilivyomaliza kidato Cha SITA sikuhitaji hata kwenda chuo. nilikuwa napenda sana hii kazi. Lakini kwa kuwa Mungu hakutaka niikose mbingu, ameuzuia mguu wangu usipige hatua kuelekea kwenye kazi iliyogubikwa na dhambi za Kila namna na Kila aina ya laana, ubugabire na kutokutumia akili zaidi ya kutumwa tumwa 24/7 kufanya ufala
Yes Mimi pia, Apunzike anapostahili RPC Tanga 2000yrs Mama Faith, alinisaidia sana kuninyima nafasi
 
Askofu Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya Wana Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula.

Je hiyo kanisa waumini wanawajibika kutaja vyama vyao?
Acha upoyoyo!
 
Huu utaratibu wa kuajiri watu kuwa plsi kwa kuangalia uwezo mdogo wa akili unaligharimu Taifa.

Tubadilishe mfumo, mtu akitaka kuajiriwa awe ni yule ambaye IQ yake siyo below average.
 
Huu utaratibu wa kuajiri watu kuwa plsi kwa kuangalia uwezo mdogo wa akili unaligharimu Taifa.

Tubadilishe mfumo, mtu akitaka kuajiriwa awe ni yule ambaye IQ yake siyo below average.
Hakika
 
Ndiyo, walikuwa wamevaa sare za chama.Kwani kuna sheria wamevunja kwa kwenda kanisani wakiwa wamevaa sare za chama?Taifa huongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria na wala siyo kwa mujibu wa hisia za watu au matamanio ya watu.

Duniani ukiwa na maarifa hutoangamia.
Hao wamekosa maarifa ndio maana wanaangamia kwenye mikono ya polisi.
Hiyo katiba mpya itaondoa vipi ujinga wa watanzania?
 
Wakuu, nimepata hii updates ila kwa kweli hata kama Polisi wetu wanatumwa basi at least watumie hata akili. Why wanalazimisha kujenga chuki isiyomithilika kwenye jamii?? Was it necessary?

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi na baadhi ya Askari Wanyama pori wanaozea gerezani kwa kufanya mauwaji Kanisani. anyways wacha niwape updates

Updates

Makamanda, habari za muda huu. Mpaka sasa hivi tunaendelea kushughulikia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama walipokuwa kwenye misa jana Kawekamo.

Walioko lock up ni Katibu wa kanda ya Victoria, Mwenyekiti wa Ilemela, Katibu wa Nyamagana na wanachama wengine jumla yao ni 20.

Baada ya kumuona OCD asubuhi ya leo, alitwambia kuwa wanatuhumiwa kwa kufanya vurugu kanisani na kwamba alipigiwa simu na viongozi wa kanisa.

Ilibidi tukauone uongozi wa kanisa Katoliki jimbo la Mwanza, tumeonana na msaidizi wa baba Askofu na akatuwezesha kuongea na askofu Mkuu Renatus Kwande.

Askofu Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya Wana Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula.

Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema.

Awali asubuhi, walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani.

Baba askofu katupa msaidizi wake tukaenda naye Kirumba na ameongea na OCD, sasa ocd kageuza kwa si kanisa lilimpigia simu bali ni waumini wawili mmojawapo anaitwa Gerlad Joseph. Msaidizi wa Askofu kawasiliana naye na sasa Askofu amemtuma katibu wake Padre Nyanda, tunaendelea kumsubiri hapa kirumba.

Msimamo wetu ni:
1. Wawaachie wote bila masharti ya dhamana.

2. Au baba Askofu akawadhamini waumini wake.

Wanzagi
Wanzagi- sikutegemea CHADEMA kuonyesha ujinga wa kiasi hiki. Mnachotaka ni kulichonganisha Kanisa hasa RC na KKKT na serikali na waumini ambao siyo CHADEMA- tunajua wakristo hupenda kuleta chokochoko pale ambapo nchi inakuwa na rais ambaye si Mkristo SASA MMEANZA.- NI UJINGA MTUPU MNAOFANYA
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Miongoni mwao kuna Wazee wa miaka 69, 70, 75

Siamini kama Jeshi la Polisi linakosa weledi kiasi hiki! Yaani ni kweli hakuna Polisi hata mmoja mwenye akili timamu za kufanya maamuzi sahihi?

Jeshi letu halina Washauri? Hakuna Wazee? Hakuna systems? Hawana miongozo? Wao wanachojua ni kukamata tu! Kweli?
Lazima itakuwa wame play victims...Kwanini wawe CHADEMA kanisani na siyo waumini kanisani? Ebu acheni kuvuruga nchi nyie watu.
 
Hapa chama kinatafuta kuunganisha Dini na Siasa ILI kuongeza uungwaji mkono tatizo walichokosea ni kuwatafuta hata wasio waumini wa dhehebu usika ajabu Waislamu na wasabato kuingia kanisani huku wakijifanya ni wakatoliki Dini Yao haiwaruhusu kwani Kuna tofauti kubwa za kiitikafi.

Chondechonde Dini iachwe
 
Wanzagi- sikutegemea CHADEMA kuonyesha ujinga wa kiasi hiki. Mnachotaka ni kulichonganisha Kanisa hasa RC na KKKT na serikali na waumini ambao siyo CHADEMA- tunajua wakristo hupenda kuleta chokochoko pale ambapo nchi inakuwa na rais ambaye si Mkristo SASA MMEANZA.- NI UJINGA MTUPU MNAOFANYA
Hawa ndugu wameamua kuvuruga nchi bila kujali chochote.
 
Back
Top Bottom