Kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM,yamejitokeza mambo mbalimbali yanayoashiria goli la mkono. Mchakato huo umeanika mambo ya kujipatia kura na kuzuia kura za wengine.
Mfano,kumeripotiwa kutolewa kwa rushwa na hata kukamatwa kwa wagombea mbalimbali. Pia,kumekamatwa kura feki Tarime na kutotangazwa kwa matokeo Buguruni. Bunda,matokeo yalitangazwa chini ya ulinzi mkali. Tena,kumetokea kupigana au kupigwa Bunda na hata Kongwa kwa Ndugai.
Wapo walioambiwa wana kadi feki Arusha na hata waliokamatwa na kadi feki Ilala. Kimsingi,mambo hayo ni mafunzo tosha kwa wapinzani kuelekea uchaguzi mkuu. Mambo hayo ndiyo mambo ya goli la mkono. Shtukeni!