Kwa mara ya kwanza niliamua kushiriki kwa karibu uchaguzi huu lakin i nimeambulia kukata tamaa kubwa sana mpaka sasa natufuta pa kutokea tu. Nashukuru leo ni jumapili na ilibidi niombewe ili niwee kurudi katika khali yangu ya kawaida
ngoja na mimi nikapige kura ndo nije humu.... naona kila mmoja ana kuja na hoja za siku nyingi na sis za leo...!
TUKAPIGE KURA.....MUDA UNARUHUSU...!
Samahani mkuu, unajua inaudhi sana, tunaposhindwa kutimiza wajibu wetu na kazi zetu kulalamika tu.Engineer! Taratibu mkuu wangu,hapo nilipobold,hayo si maneno ya hadhi ya Engineer,unajuaje kama hatujapiga kura?
nampongeza mwana mama fulani hivi kwa kujitolea kwa hali na mali kuzunguka maeneo mengi kuwapigia debe wagombea wake; huyu mwanamama aliwahi kugombea ubunge na wakachuana vikali na nzansugwanko (mb)}
Nawasilisha....
Wakuu tupeane updates
Mie nimetoka kupiga kura lakini,nimeshindwa utaratibu ni mbaya kupita kiasi.
Oroadha ya majina ya wapiga kura ambayo ilibandikwa jana imelowa yote na mvua ya jana-mpaka sasa zoezi zima la kupiga kura bado alijaanza-na kwa maaantiki hii watu wengi sana awatapiga kura leo kutokana na kasoro za urodheshaji wa majina kwenye mbao za vituo.
Mimi ni natakiwa nipige kura Buguruni Kisiwani-kwa mantiki hii sipewi fursa ya kuchagua mwenyekiti wa serikari ya mtaa wangu ,kwa sababu ya uzembe wa watendaji katika Manispaa husika.
Naomba update mitaa mingine.
Mdau wa Lusungo Ipinda Kyela.