Updates: Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Updates: Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Madega.jpg

Wakati uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukitarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma, hatimaye nafasi ya urais wa shirikisho hilo imepata wapinzani wawili hadi sasa.

Jamal Malinzi ambaye ni rais wa sasa wa shirikisho hilo amechukua fomu ya kutetea nafasi yake lakini amepata mpinzani.

Muda mfupi baada ya Malinzi kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo, ndipo mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga, Iman Madega naye akatinga maguu kwenye ofisi za shirikisho hilo kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania urais wa TFF.

Madega amechukua fomu hiyo leo asubuhi katika ofisi za shirikisho zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, hiyo ni dalili njema kwa wanamichezo ambapo awali ilionekana kama Malinzi hatakuwa na mpinzani katika nafasi yake.

Malinzi ndiye anayeshikilia kiti hicho kwa takribani miaka minne iliyopita.
Amekuwa akishutumiwa kushindwa kusaidia kupatikana kwa mabadiliko.
Hata hivyo, yeye amekuwa akisisitiza kwamba amefanya mengi.

Leo amechukua fomu kuthibitisha kuwa atawania miaka minne ijayo

Habari kwa Hisani ya Salehe Jembe
 
Kuna watu ambao siku zote wanawaza uongozi, zikitokea nafasi za uongozi popote, lazima yumo, iwe kwenye siasa au michezo, mfano mzuri ni huyu Madega. Madega aliwahi kuwa mwenyekiti wa Yanga (sijui aliacha alama gani), baadae akagombea ubunge, sasa anagombea TFF.

Kupitia hilo naanza kujiuliza, hivi kuna watu wanaamini kuwa maisha yao ni kuongoza tu?

Vv
 
So far wote waliojitokeza wana nasaba za Yanga wa Kimataifa. Wote waili walikwahi kuwa viongozi wa Yanga.

Muda ndiyo huu, hao wenye nasaba za matopeni wajitokeze ili wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF waje watende haki. Au hakuna wenye sifa. Jaribuni kumshawishi Komandoo wenu Hassan Dalali ajitokeze. Wapi Kaburu? Naye Bi. Hindu hana sifa?

Hizi kelele za Malinzi au sasa Madega anaipendelea Yanga ziiishe
 
Basi sawa tutarajie upinzani kwenye huo uchaguzi wa TFF
 
Back
Top Bottom