Nipo Coco beach na Wana familia wangu ninaoishi nao kwa Sasa!
Hii ni mbinu yangu kongwe kudhibiti waruka fensi na kwenda kusikojulikana usiku wa Mikesha
Hapa ni Kama Jeshini kwangu ni mwendo wa kuhesabu namba, najua wapo wanaonilaani sana lakin ni kwa Nia njema tu!
Tumezungusha Mduara wa Viti na Soft drink na Kahawa kwa sie wengine na kibaridi hiki japo kwa pemben yetu kizazi cha Firauni nacho hakijaadimika wapo
Nyakati hizi huwa pia najikumbusha Ndugu na Jamaa zangu ambao Miaka ya Nyuma tarehe Kama Hii tulikuwa nao eneo hili Miaka kadhaa iliyopita lakin Leo Hii miili Yao ni sehemu ya Matabaka ya udongo