Lamborghini Urus SE
Wakali kutoka Italy, Lamborghini wametuletea plug in hybrid (PHEV) ya kwanza kutoka kwao
Lamborghini Urus SE, ambayo ni SUV.
Hii ni kwa wanajamiiforums waliokataa kununua Lamborghini kwa kisingizio inakunywa sana mafuta, Haya Hybrid hii hapa, ina average consumption ya 12 L/100km (8.3 km/L)
View attachment 2976753
Urus SE ina twin-turbo 4.0L V8 engine ikiwa na mota za umeme ambazo kwa pamoja zinakupa horse power 800, na maximum speed ya 312 km/h. Urus kwenye EV range inaweza kufika hadi 60km.
View attachment 2976754
Design ya Urus ni unyama, kwanza wameleta muundo mpya wa taa za LED, wamebadirisha muonekano wake wa mbele kuanzia grille na bumper, na nyuma wamesema design imekua inspired na Gallardo (Hii ilikua model ya Lambo miaka ya 2003 hadi 2013).
View attachment 2976755
Ndani utajiona kama pilot wa jet fighter, kuna 12.3-inch touchscreen ikiwa na upgraded "Human Machine Interface" (HMI).
View attachment 2976761
Lamborghini wanasema Urus SE imepunguza madhara kwenye mazingira kwa silimia 80 ukifananisha na model iliotangulia.