Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Genesis G80 EV
Genesis ni sub brand ya Hyundai inayotengeneza Luxury cars. Genesis kuna vyuma vikali unaweza usiamini vimetoka kampuni ya Hyundai. Ni kama Maybach ya Mercedes Benz au Lexus ya Toyota.

Sasa nao wamezindua G80 EV sedan ya umeme kwenye maonesho aya.

 
BMW watambulisha 2nd Generation ya X2

BMW wametambulisha generation ya pili ya SUV BMW X2. Generation ya kwanza ilikua F39 na sasa ni U10. Kawaida BM uwa hawabadirishi saaana interior na exterior kutoka generation moja kwenda nyingine ila sasa hivi wametisha. Big changes, inside and outside.

Kwanza ni kubwa, na unaweza ona kwenye picha ata 20 inch rims zinaonekana ndogo.

Inaitwa X2 M35i ila sio M car. Huu mchezo wa kuweka a powerful letter M kwenye grille au nyuma imekua kawaida kwa BMW siku hizi. Tumeona kwenye X1 M35i pia.


Ndani unyama umeendelea, wameweka seat za M cars, ambazo zamani kuzipata ilikua mtiti.

Mengine hayajawekwa wazi ila X2 sio best selling SUV ya BMW tunasubiria mwezi June ambapo wajerumani watatangaza next generation ya best selling SUV BMW X3 iitwayo G45.

Hii G45 ndio itakua first BMW kua na iDrive 9 na itakua na separate infotainment rotary knob.

Okay all the best BM.

PS: Sijui pia kama hii X2 itakua success kwasababu wenyewe wanajipinga, wametoa na iX2 ambayo ya umeme sasa unategemea nan ataenda petroleum?
 
C16 kutoka kwa Leap Motoros
Hii ni SUV + MPV kutoka kwa kampuni la Kichina Leap Motors.
Kwanza nje ina muonekano wa kibabe.



Inakuja na options mbili, either Hybrid au full EV.
EV ina electric motor yenye 215 kW na battery lenye 67 kWh (Lithium Iron Phosphate battery) ila imenyimwa speed maximum ni 160kph na ina range ya 520 km ukipiga full charge.
Inakuja na fast charge capabilities unaweza chaji kutoka 30% to 80% ndani ya dk 15 tu.

Ukitaka Hybrid inakuja 4 cylinders engine yenye 1.5L, 170kW motor na battery dogo lenye 28kWh. Top speed ni 170km/h na ukiweka EV tu itatembea tu 230km.


Mbele ina screen ya inch 14 ikiwa na OS (Operating System) ya LEAP, na Snapdragon 8295 SoC.

Seat ya nyuma, tunawapa screen kubwa ya inch 15 waenjoy maisha.

Ukiangalia layout ya seat ni 2+2+2 ndio maana jamaa hawaiti SUV ila wanaita SUV+MPV.


NB: Leap Motors wanasema wamepokea orders 19,000+ ndani ya masaa 24 tokea waitangaze hii chuma.
 
EV's zote ni zero noise yaani hapa ni mwendo kama upo chumbani Tu.
Haya magari utapata mlio kutokea kwenye matairi Tu
daraja la kigamboni

Nilitaka kupata jibu hili mkuu.

Sasa tuje kwenye real life ya kiafrika humu barabarani je, inawezekana kwa kiasi gani kuendesha chombo hakina sauti mtaani 🙂?.
 
CATL (kampuni la kutengeneza battery za EV)

Hawa hawana gari ila wamwkuja na habari njema. Wamezindua technology ya battery kwa kuongeza speed ya kuchaji (4C) na ndani ya dakika 10 za kuchaji unaweza kuongeza kilometa 600, na pia wamefika range ya kilometa 1000.
 
H
Hivi haya magari ya umeme unachaji popote hata nyumbani kwako au sehemu maalum?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…