C16 kutoka kwa
Leap Motoros
Hii ni SUV + MPV kutoka kwa kampuni la Kichina Leap Motors.
Kwanza nje ina muonekano wa kibabe.
Inakuja na options mbili, either Hybrid au full EV.
EV ina electric motor yenye 215 kW na battery lenye 67 kWh (Lithium Iron Phosphate battery) ila imenyimwa speed maximum ni 160kph na ina range ya 520 km ukipiga full charge.
Inakuja na fast charge capabilities unaweza chaji kutoka 30% to 80% ndani ya dk 15 tu.
Ukitaka Hybrid inakuja 4 cylinders engine yenye 1.5L, 170kW motor na battery dogo lenye 28kWh. Top speed ni 170km/h na ukiweka EV tu itatembea tu 230km.
Mbele ina screen ya inch 14 ikiwa na OS (Operating System) ya LEAP, na Snapdragon 8295 SoC.
Seat ya nyuma, tunawapa screen kubwa ya inch 15 waenjoy maisha.
Ukiangalia layout ya seat ni 2+2+2 ndio maana jamaa hawaiti SUV ila wanaita SUV+MPV.
NB: Leap Motors wanasema wamepokea orders 19,000+ ndani ya masaa 24 tokea waitangaze hii chuma.