Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Bado Wanajeshi nao wanaendeleza ujinga, mwenzao kauwawa na kijana Kato na kijana ameshakamatwa na tukio lilihusisha watu wawili, kuna sababu gani kwenda mtaani kupiga raia na kuonea wengine wasio na hatia?..

Tabia hii wanaoifanya hawa wajeda ndio ileile iliyosababisha mwenzao kuawawa na wao wanaiendeleza, inaonyesha jeshi letu kuna mahala limekosa nidhamu.

Hizi hasira, ukakamavu, sifa nk wanapaswa kwenda kuzionyesha front line na sio kuonea raia wasio na mafunzo yeyote ya kijeshi.
 
kumtukana mtu na kwenda kumtandika makofi kisa kakwambia upishe apite umeziba njia, shida ilianzia hapa.

Sio kila binadamu anakubali uonevu, Mjeda alivuka mipaka pale alipokwenda kumnasa vibao kijana wa bajaji.
Sasa kamuuwa sababu ya kupigwa makofi amepata nini? yule kafa na yeye maiti bado inatembea tu faida yake ni nini? Kama tunaona sawa ukionewa tu na wewe malizia basi huku mijini nadhani kila siku, kila sasa kuna mtu angekuwa anauliwa maana uonezi kila sehemu upo. Ndio maana nimesema funzo kujifunza ku control hasira zetu hata ukiwa umeudhiwa kiasi gani. angefanya na yeye kumpa kipigo yaani yeye kapigwa makofi sasa yeye angempinga mangumi lakini sio kumchoma mtu ukijuwa kabisa kitendo chako unaweza kumuuwa mtu.
 

sio kila mtu anapenda kuonewa au kudhulumiwa, hatufanani kwenye uumbaji.

asingefanya hivyo pia inawezekana angekufa kwa kihoro kwa kuwaza kila siku kwanini anaonewa.

Mauaji ya hivi pia ndio huleta haki kwa mamlaka kuona kuna umuhimu wa kuweka sheria za haki kabisa ili yeyote akionewa na yeyoye hata awe na nguvu kiasi gani basi sheria iweze kufanya kazi.

Mamlaka zinapaswa kusimamia sheria ili zifanye kazi kwa kila mtu na dola inapaswa kulinda kila mtu
 
Sheria gani unaongelea hapa? ok tuseme sheria zifuatwe. Wewe mtu kakupiga utafanya nini? sheria inasema nenda kashtaki police hakuna sheria inasema lipiza kisasi ukionewa wewe malizia uwa kabisa. Nchi inasheria issue zinafuatwa au la hiyo hoja nyingine. Unajuaje kama kaonewa? kama alimtukana matusi ndio sababu ya kupigwa makofi? kwani maudhi mpaka mtu akupige kuna watu mdomo tu anaweza kukupandisha hasira. Kama nilivyosema yeye kidume hakubali kuonewa sasa yupo wapi? kauwa na huu ndio mwisho wake.
 
Na wewe acha ujinga,aliyesababisha yote hayo ni huyo mpumbavu Kanali! Angekuwa mwadilifu na mwenye busara amani angekuwepo na hakuna kitu kibaya kingemtokea!
Wewe sijui unasimamia nini? Sheria zipo na watu wote wanapaswa kufuata!
Kujificha kwenye kichaka cha kuudhi na kukera watu na kuamini kwamba ili wapate haki lazima waende polisi ni ujinga!
Polisi yupo kwa ajili ya ulinzi na usalama lakini usalama na ulinzi unaanzia kwako!
Huyo mjeda limbukeni wa cheo mwache amevuna alichopanda na kuna uwezekano ni tabia yake ya mda mrefu!
Hakuna jeshi bila wananchi na ni jeshi la wananchi huyo mjeshi kaaibisha jeshi!
Kitabu chake kimefungwa na hakuna la maana cha kumtetea zaidi ya kujifunza kuwa na nidhamu!
 
Safi sana najua watatupiga ila wameshajifunza

Jasiri mwongoza njia kato
 
Basi unajikuta bonge la mchunguzi kumbe ni ----
 
Sasa huyo aliyeuwa ndio unadhani utamuona mtaani? jinga kubwa wewe, unadhani sote tungekuwa tukiudhika tu tunauwa angebaki mtu mtaani, si tungechinjana kila siku. Pumbavu akili za kichawi...
 
Kwa ujumla naona nchi haina jeshi la kutegemewa kwa sababu jeshi hawana nidhamu na siku zote usipokuwa na nidhamu kupigwa ni rahisi sana. Jeshi kitu cha kwanza ni nidhamu na nidhamu ni kuwaheshimu wote wakubwa na wadogo, matajiri na maskini. Ila kwa kusoma ili andiko na kuelewa nimeona jwtz halina nidhamu kwa maana hiyo Tanzania haiko salama.
 
Achana nao hawajui walitendalo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…