Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Jeshi halipaswi kabisa kujenga bifu na raia..
Vinginevyo kikinuka, raia wanaweza kuwa upande wa maadui kama ilivyotokea kwa jeshi la Uganda ambapo raia wengi wa Uganda walikuwa upande wa jeshi letu kutokana na kwamba walichoshwa na vitendo vya kionevu na ubabe vya UPDF ya kipindi hicho cha Hayati Alhaj Idd Amin Dada
 
Kuna umuhimu wa kupitia usajili wa kila boba boda Na Bajaji ndani ya hii nchi ili kila mmiliki ajulikane na hii itapelekea hiyo biashara kuwa ki professional.
Sasahivi udhibiti ni mdogo sana mtu amepata ela anagawa boda boda au Bajaji kwa mtu hajui nyumbani kwake hakuna dhamana yoyote imewekwa kwa lolote likitokea matokea yake wizi unaingizwa ndani yake .
Faini za awali ziliponguzwa zirudishwe ama sivyo madhara makubwa yataongezeka kwa watumiaji na abiria .
 
Mimi ngumi ni kitu cha mwisho kabisa hata kufikiria kurusha. Kuna watu hata gari kugusana tu tayari anashuka ngumi mkononi! Kuna watu hata humfikirii lakini ni hatari kwenye hand to hand unaweza kutia aibu na mwili wako.

Mpenda ugomvi yeyote ni vile hajakutana na kisiki kimnyooshe ndio ataanza kwenda taratibu na watu.
 
Kwa mwanaume anayejitambua hapo palikuwa siyo pakuonyesha ubabe,ukiwa na familia epuka sana shari huyo unayemletea shari anaweza kuwa yupo vizuri kuliko wewe ukaumbuka mbele ya mkeo na wanao.

Tuachane na kumuua tu-assume kwamba Bajaj driver Kato angekuwa yupo vizuri kurusha mkono akampasua hiyo familia yake ingemuonaje?mkewe wangepishana kauli siku amwambie mwanaume gani wewe unajifanya una mafunzo ya kijeshi unapigwa na dereva wa Bajaj asiyejua hata kushika bastola?bado angethubutu kusema mkewe ana dharau?maana hayo angekuwa ameyataka yeye.
Nakazia.
 
Huko kazini Kwa Muna huenda walikuwa wanagombea hicho cheo kiasi cha kurogana.

Hivi ina raha gani kama hivyo mwenzio kafa wewe upewe hiyo nafasi yake Halafu utapata amani na furaha Kweli kwenye nafsi na moyo wako?
Labda iwapo dhamiri yako ilishakufaga! [emoji848][emoji848]
 
Sema ana uandishi mbaya sio mwandiko mnaya. Mwandiko hauusiani na alama za uandishi na upangaji wa maandishi.
Mwandiko ni muunganiko wa herufi tu, na upo wa kuchapa na kuunga wengine huita mcharazo na wima..
Mwandiko mbaya ni ule usiosomeka .
Je mwandishi mwandiko wake hausomeki ?
Mpo wengi sana mnaoshindwa kutofautisha mwandiko na uandishi.
Soma la Insha lilikupita kushoto ila unajifanya unajua kukosoa.
Huwa sipendi mnavyochanganya insha na mwandiko? Mwandiko ni 'subset" ya insha
UANDISHI !UANDISHI!
Ndio maana wanahabari wanaitwa waaandishi wa habari hawaitwi wanamwandiko wa habari, kwa sababu wanaandika habari sio mwandiko( mwandiko ni tool ).
Mwandiko ni art of making letters.
Mwandiko ni somo la chekechea na drs la kwanza.
Uandishi in sanaa ya kuunda maneno ssentensi a insha kwa kuzingatia kanuni zote za uandishi.
Picha hii ni somo la kusoma na kuandika. Mtoto ataunda hizo herufi bila kujali zinaleta maana au la na baadae kuunganisha ili kipata maana na kusoma maneno yatayoundwa na herufi hizo.

View attachment 2795446View attachment 2795446
Asante kwa kuamua Kutenga muda wako Kulielimisha hilo Pumbavu la Milele Medecin ila usitegemee kama litakuelewa kwani Limerithi huo Upumbavu wa Milele unaomgharimu.
 
Japo kuna vitu vime ongezwa kwenye hii story lakini sawa, Mwisho wa siku Mwanajeshi kazi yake ni kifo japo tumekula hasara hajafia kazini. Nidhamu na Utii viwe mbele katika yote
 
Kuna umuhimu wa kupitia usajili wa kila boba boda Na Bajaji ndani ya hii nchi ili kila mmiliki ajulikane na hii itapelekea hiyo biashara kuwa ki professional.
Sasahivi udhibiti ni mdogo sana mtu amepata ela anagawa boda boda au Bajaji kwa mtu hajui nyumbani kwake hakuna dhamana yoyote imewekwa kwa lolote likitokea matokea yake wizi unaingizwa ndani yake .
Faini za awali ziliponguzwa zirudishwe ama sivyo madhara makubwa yataongezeka kwa watumiaji na abiria .
Umeandika ukiwa na bia ngapi kichwani!??
 
Mimi ngumi ni kitu cha mwisho kabisa hata kufikiria kurusha. Kuna watu hata gari kugusana tu tayari anashuka ngumi mkononi! Kuna watu hata humfikirii lakini ni hatari kwenye hand to hand unaweza kutia aibu na mwili wako.

Mpenda ugomvi yeyote ni vile hajakutana na kisiki kimnyooshe ndio ataanza kwenda taratibu na watu.
Sawa sawa, mkuu
 
Haya mambo nasikiaga kama story tu. Bado huwa siamini unaweza ukawa umekaa zako ukaja ukaanza kupigwa kisa kuna mtu mwingine huko kafanya makosa..

Sasa kwa karne hii ya Technology, what if mtu akachukua video?? Kwa kweli sidhani kama ni kweli raia wanaweza kupigwa bila kosa
 
Back
Top Bottom