Updates za Mazao ya msimu wa 2022

Updates za Mazao ya msimu wa 2022

huku tarime bado mvua zinaendelea kunyesha kwa kiasi chake, tulivuna mwezi wa tatu, hapa tunasubiri tuvune Tena mwezi wa saba
 
Mwaka huu sikuwaza kuingia shambani kabisa,ila zile mvua za May nilizitumia ipasavyo nilipanda milimao size ya kati mpaka muda huu yote imeshika na naomba naomba mvua za Vuli zianze mapema ishamili zaidi ili mwakani ikimpendeza Mnyazi niipige kisu.
Umepandia wapi mkuu, mwaka huu hata wale waliojaribu Kupanda milimao saizi kubwa, wameangukia pua
 
Afadhali ya nyie kama mtavuna kidogo wengne kwenye mpunga tumekula za kichwa mazima aisee... alaf ndio bei ya mpunga kubwa hatar.
Ngoja tukanunue tu alzeti ili tufidie hasara japo nao mwaka huu wameanza na bei kubwa balaa.
Sehem gani mkuu maana sisi tumelima Morogoro huko mlimba Hali c mbaya Sana Na Bei imechanganya hatari
 
Mwaka huu sikuwaza kuingia shambani kabisa,ila zile mvua za May nilizitumia ipasavyo nilipanda milimao size ya kati mpaka muda huu yote imeshika na naomba naomba mvua za Vuli zianze mapema ishamili zaidi ili mwakani ikimpendeza Mnyazi niipige kisu.

Kuipiga kisu ndio kufanyaje mkuu...?
 
Kwa sasa baadhi ya mazoa kwa SONGEA -Ruvuma yameanzwa kuvuna ikiwemo ufuta,soya , mpunga na mahindi.Kwa upande wa maharage kwa soko la sodeko yanaonekana yapo mengi na kufanya Bei Hadi wiki iliyopita unaweza pata kwa Tsh 1000
Ni maharage ya aina gani yanapatikana huko
 
Mvua zimegoma kabisa mwaka huu...mpunga umekataa kabisa..nimeamua kupanda viaz na mahind kidogo ya kumwagilia.....najipanga nipate pesa nichimbe kisima, mvua imenifanya mbaya sana
vipi gharama za uchimbaji kisima zipoje
 
Wapi huko ambako kijiji gani debe la alizeti lipo chini ya 9000 kwa sasa, napatafuta sana mmoja anijibu basi na bei yake. Nipo Mbeya kwa sasa nimekutana na bei ya 10,000 kwa hapa karibu karibu na mimi.
 
Naulizia Soyabeans wapi nitapata na bei iko vipi.?
 
Back
Top Bottom