Upekee tunaoutaka wana Simba SC ni kuwa Bingwa wa CAFCL na Super League siyo kuzindua Jezi Mlima Kilimanjaro

Upekee tunaoutaka wana Simba SC ni kuwa Bingwa wa CAFCL na Super League siyo kuzindua Jezi Mlima Kilimanjaro

Sijaona bado ulazima huo wa Kujihangaisha kwenda Kileleni Mlima Kilimanjaro na Kuzindua Jezi zetu Simba SC ili tu Kufunika tukio la Yanga SC kwa Wao Kuzindua zao Ikulu ya Malawi mbele ya Marais Wawili wa Malawi na Tanzania.

Na si lazima kila Yanga SC ikija na Kitu kipya cha Ubunifu basi na Sisi Simba SC tuanze Kulazimika kutafuta Tukio la Kuwafunika Yanga SC na tuzungumzwe Simba SC tu.

Haya tumejipanga na hadi Kutangaza kuwa Jezi zetu Simba SC tunaenda Kuzindulia Kileleni Mlima Kilimanjaro na Tukio kuwa televised na Azam Tv je, ikitokea Siku hiyo hali ya Hewa ya huko Mlimani ikabadilika na kuwa mbaya au si rafiki hizo Jezi zetu tutazindundulia wapi?

GENTAMIYCINE naheshimu mno na sana Ubunifu wa Matukio mbalimbali ya Simba SC na napenda kuona Ubunifu zaidi ila sipendi Ubunifu wa Kishamba, Kienyeji na wenye Mhemko kwani mnaweza kudhani mnaingarisha Simba SC Kimatukio kumbe ndiyo mkawa mnatuanika wana Simba SC wote ( GENTAMIYCINE nikiwemo ) kuwa ni 'Mapimbi' kweli kweli na tukaanza Kuchekwa na Watani zetu Yanga SC.

Na nimetoka kutizama Weather Forecast ya Ijumaa ijayo Siku ya Tukio itakuwa ni Baridi Kali na Mawingu kule Kileleni hivyo naona kabisa kama Msemaji Wetu Simba SC Ahmed Ally ndiyo atapanda kule juu na Jezi zetu mpya anaweza asirejee mazima, huku Cameraman wa Azam Tv nae Pumu ( Asthma ) ya ghafla Kumkamata na Kushindwa kuchukua Matukio yote muhimu.
We jamaaa daah, salute[emoji2][emoji1787]
 
Waambie waniongezee BAN nyingine ili ufurahie zaidi sawa? Halafu umeshajiuliza ni kwanini hata GENTAMIYCINE nikiwa BANNED kwa Siku, Wiki, Mwezi na Miezi bado tu naendelea Kujadiliwa na kuwa na Mvuto wangu ule ule hapa JamiiForums?

Hawezi kamwe kupewa Tunu ( Shani ) Kuu Nne ( 4 ) tukuka za kuwa......

1. Purely Talented
2. Charismatic Fella
3. Game Changer
4. Entertainer

Halafu usiwe Kipenzi cha Members hapa JamiiForums na Chukizo kwa Wapumbavu na Waswahili wa mfano wako.

Utajiri mkubwa wa Followers 158 nilionao hapa JamiiForums ni Jibu tosha kuwa nina Thamani ya Kipekee na Mvuto usio wa Kifani kwa Wasomaji huku Wapumbavu mnaopoteza muda Wenu Kutwa Kunichukia, Kunishambulia, Kunidhalilisha na Kunitukana hapa JamiiForums mkiwa ndiyo Watu mnaosaidia Kuniongezea Umaarufu wangu hadi Kujadiliwa ndani na nje ya JamiiForums.

Asante Mwenyezi Mungu.

Mimi ndiyo GENTAMIYCINE The King!!!!
Heshima imefuata mkondo wake, that is the point

Umekuwa mtoto mzuri sasa hivi
 
Back
Top Bottom