Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa milima yenye vilele virefu zaidi Duniani. Mlima huu una sifa nyingi zinazoutofautisha na milima mingine, sifa hizo ni pamoja na:
1. Ni miongoni mwa milima saba enye vilele virefu zaidi Duniani. Lakini pamoja na kuwa hivyo bado ni mlima rahisi kupandwa ukilinganisha na milima mingine kwa sababu hauhitaji utaalamu mwingi wala vifaa vingi vya kisasa kama kamba, shoka la kujishikiza kwenye barafu n.k. Inawekewa kwenye kundi la milima ya kupanda kwa kutembea.
2. Ni mlima uliojitenga na kusimama wenyewe pasi na safi za milima tofauti kabisa na milima mingine Duniani.
3. Mlima huu upo karibu zaidi na mstari wa Ikweta, Ikweta ni mstari wa kufikikirika wenye nyuzi sifuri unaogawa Dunia katikati katika pande mbili yaani Kaskazini na Kusini.
Mlima huu kulingana na vipimo vya kijiografia upo umbali wa maili mia mbili na tano (205) kutoka ulipo mstari wa Ikweta.
4. Mlima huu una kuni tatu za kivolkano ambazo ni;
(i) Kibo 5895m
(ii) Mawenzi 5149m
(iii) Shira 3962m
5. Mlima huu ni wa kivolcano, volcano tuli.
6. Zaidi ya nusu ya watu wanaojaribu kupanda mlima huu hushindwa kutokana na kupita ruti mbaya au matatizo ya upumuaji kutikana na mwinuko kutoka usawa wa bahari.
7. Watu wenye umri mkubwa na watoto wamefanikiwa kupanda na kufika katika kilele cha mlima huu. Kwa mfano, Mwaka 2019 Mwanamke wa Kimarekani Anne Lorimo aliyekuwa na umri wa miaka 89 alifanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro huku mwaka 2018 Mtoto wa Kimarekani wa miaka sita Coaltan Tunner alifanikiwa kufika katika kilele cha mlima huu.
8. Safari ya kupanda mlima huu ni kama kutoka kwenye Ikweta kwenda Antaktika.
Unaweza ukatafakari kupitia picha hizo hapo chini.
Karibu.