Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
BuhhhhhhhhhJe kuna uwezekano wa kuhamishia huu mlima kule Burigi-Chato ili ukaipe sapoti ile mbuga pendwa ya mwendazake? Pale kwenye kitovu cha utalii kwa kanda ya ziwa?
Sure.The highest stand alone mountain in the world...
Very Beautiful.Mawenzi peak. Hapa ni uwanja wa shule za msingi Tarakea & mbomaiView attachment 1765031
MÊmENtO HoMO
Mlima Kilimanjaro si miongoni mwa milima saba yenye vilele virefu zaidi duniani.Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa milima yenye vilele virefu zaidi Duniani. Mlima huu una sifa nyingi zinazoutofautisha na milima mingine, sifa hizo ni pamoja na:
1. Ni miongoni mwa milima saba enye vilele virefu zaidi Duniani. Lakini pamoja na kuwa hivyo bado ni mlima rahisi kupandwa ukilinganisha na milima mingine kwa sababu hauhitaji utaalamu mwingi wala vifaa vingi vya kisasa kama kamba, shoka la kujishikiza kwenye barafu n.k. Inawekewa kwenye kundi la milima ya kupanda kwa kutembea.
2. Ni mlima uliojitenga na kusimama wenyewe pasi na safi za milima tofauti kabisa na milima mingine Duniani.
3. Mlima huu upo karibu zaidi na mstari wa Ikweta, Ikweta ni mstari wa kufikikirika wenye nyuzi sifuri unaogawa Dunia katikati katika pande mbili yaani Kaskazini na Kusini.
Mlima huu kulingana na vipimo vya kijiografia upo umbali wa maili mia mbili na tano (205) kutoka ulipo mstari wa Ikweta.
4. Mlima huu una kuni tatu za kivolkano ambazo ni;
(i) Kibo 5895m
(ii) Mawenzi 5149m
(iii) Ashira 3962m
5. Mlima huu ni wa kivolcano, volcano tuli.
6. Zaidi ya nusu ya watu wanaojaribu kupanda mlima huu hushindwa kutokana na kupita ruti mbaya au matatizo ya upumuaji kutikana na mwinuko kutoka usawa wa bahari.
7. Watu wenye umri mkubwa na watoto wamefanikiwa kupanda na kufika katika kilele cha mlima huu. Kwa mfano, Mwaka 2019 Mwanamke wa Kimarekani Anne Lorimo aliyekuwa na umri wa miaka 89 alifanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro huku mwaka 2018 Mtoto wa Kimarekani wa miaka sita Coaltan Tunner alifanikiwa kufika katika kilele cha mlima huu.
8. Safari ya kupanda mlima huu ni kama kutoka kwenye Ikweta kwenda Antaktika.
Unaweza ukatafakari kupitia picha hizo hapo chini.
Karibu.
View attachment 1764928
View attachment 1764929
View attachment 1764930
View attachment 1764931
View attachment 1764932
hapo shimoni au crater mgeni akiomba kulala hapo analipia extra fees achana na mziki wa hapo ni kirambasi babaa!!hata masoja wanapakimbia!!
Mkuu hivi hiyo crater ni ya asili au mlichimbachimba kidogo?hapo shimoni au crater mgeni akiomba kulala hapo analipia extra fees achana na mziki wa hapo ni kirambasi babaa!!hata masoja wanapakimbia!!
kawaida wageni wengi hupewa certificate wakifika STELLA,GILMANS na UHURU ndio mwisho.ila kuvuka hapo uingie crater ni habari ingine.
ile mlima ndogo ya mawenzi huwa haipandwi au lbd kwa special sana..pale ni mziki mwingine roho mkononi na kukipanda ni vifaa maalumu
Ya asiliMkuu hivi hiyo crater ni ya asili au mlichimbachimba kidogo?
Mkuu hii picha ulipiga ukiwa kwenye ndege??
Mungu Fundi sana!Ya asili
Mkuu hapo naona kuna kuchanganya kidogo.Mlima Kilimanjaro si miongoni mwa milima saba yenye vilele virefu zaidi duniani.
Milima kumi yenye vilele virefu zaidi duniani yote ipo katika bara la Asia.
Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa milima saba iliyo mirefu zaidi katika mabara iliyomo hiyo milima.
Kuna tofauti kubwa hapo.
Himalaya ni ranges, safu ya milima, kama vile safu nyingine za milima duniani Alps Ulaya, Andes South America, Rockies North America, Drankensberg in Southern Africa, Atlas in North Africa, Ruwenzori on the border of DRC and Uganda.Mkuu hapo naona kuna kuchanganya kidogo.
Labda nikuulize swali, Kuna tofauti gani kati ya Evarest na Himalaya? Hapo kipi ni mlima?
Analala sehemu gani? Ndani kabisa ya hiyo crater au inakuaje?hapo shimoni au crater mgeni akiomba kulala hapo analipia extra fees achana na mziki wa hapo ni kirambasi babaa!!hata masoja wanapakimbia!!
kawaida wageni wengi hupewa certificate wakifika STELLA,GILMANS na UHURU ndio mwisho.ila kuvuka hapo uingie crater ni habari ingine.
ile mlima ndogo ya mawenzi huwa haipandwi au lbd kwa special sana..pale ni mziki mwingine roho mkononi na kukipanda ni vifaa maalumu
Uko sahihi.Himalaya ni ranges, safu ya milima, kama vile safu nyingine za milima duniani Alps Ulaya, Andes South America, Rockies North America, Drankensberg in Southern Africa, Atlas in North Africa, Ruwenzori on the border of DRC and Uganda.
Kwenye range ya milima unapata milimamingi, kama range ya Himalaya ina milima kama Everest na K2.
Ukitafuta milima kumi mirefu kabisa duniani, hutaukuta mlima Kilimanjaro.
Miima hii yote ipo bara la Asia.
Mlima Kilimanjaro utaupata katika milima saba mirefu kabisa katika kila bara, kwa kuwa ni mlima mrefu kabisa Africa.
Hivyo, usichanganye mambo na kusema mlima Kilimanjaro ni kati ya milima saba mirefu kabisa duniani.
Milima kumi mirefu zaidi duniani yote ipo Asia.