Upekee wa Mlima Kilimanjaro

Hii view ni ukiwa upande wa huku rombo Tarakea.

MÊmENtO HoMO
 
Mlima Kilimanjaro si miongoni mwa milima saba yenye vilele virefu zaidi duniani.

Milima kumi yenye vilele virefu zaidi duniani yote ipo katika bara la Asia.

Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa milima saba iliyo mirefu zaidi katika mabara iliyomo hiyo milima.

Kuna tofauti kubwa hapo.
 
Karibuni Kilimanjaro wakuu

MÊmENtO HoMO
View attachment 1765035
hapo shimoni au crater mgeni akiomba kulala hapo analipia extra fees achana na mziki wa hapo ni kirambasi babaa!!hata masoja wanapakimbia!!
kawaida wageni wengi hupewa certificate wakifika STELLA,GILMANS na UHURU ndio mwisho.ila kuvuka hapo uingie crater ni habari ingine.
ile mlima ndogo ya mawenzi huwa haipandwi au lbd kwa special sana..pale ni mziki mwingine roho mkononi na kukipanda ni vifaa maalumu
 
Mkuu hivi hiyo crater ni ya asili au mlichimbachimba kidogo?
 
Mkuu hapo naona kuna kuchanganya kidogo.
Labda nikuulize swali, Kuna tofauti gani kati ya Evarest na Himalaya? Hapo kipi ni mlima?
 
Mkuu hapo naona kuna kuchanganya kidogo.
Labda nikuulize swali, Kuna tofauti gani kati ya Evarest na Himalaya? Hapo kipi ni mlima?
Himalaya ni ranges, safu ya milima, kama vile safu nyingine za milima duniani Alps Ulaya, Andes South America, Rockies North America, Drankensberg in Southern Africa, Atlas in North Africa, Ruwenzori on the border of DRC and Uganda.

Kwenye range ya milima unapata milimamingi, kama range ya Himalaya ina milima kama Everest na K2.

Ukitafuta milima kumi mirefu kabisa duniani, hutaukuta mlima Kilimanjaro.

Miima hii yote ipo bara la Asia.

Mlima Kilimanjaro utaupata katika milima saba mirefu kabisa katika kila bara, kwa kuwa ni mlima mrefu kabisa Africa.

Hivyo, usichanganye mambo na kusema mlima Kilimanjaro ni kati ya milima saba mirefu kabisa duniani.

Milima kumi mirefu zaidi duniani yote ipo Asia.
 
Analala sehemu gani? Ndani kabisa ya hiyo crater au inakuaje?
 
Uko sahihi.
je, uliwahi kujaribu kuupanda Kilimanjaro?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…