Upelelezi kesi ya ‘Mfalme Zumaridi’ haujakamilika, wawili watoka kwa dhamana

Upelelezi kesi ya ‘Mfalme Zumaridi’ haujakamilika, wawili watoka kwa dhamana

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
mfalmepicc.jpg

Upelelezi wa kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu inayomkabili Diana Bundala ‘Mfalme Zumaridi’ haujakamilika, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mwanza, imeelezwa leo Alhamisi, Aprili 14, 2022.

Zumaridi na wafuasi wake 83 wanakabiliwa pia na shtaka la kushambulia na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao na kufanya kusanyiko lisilo na kibali.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Emmanuel Luvinga ameiambia Mahakama kuwa upelelezi wa baadhi ya mashtaka haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 28, 2022 itakapotajwa tena.

Washtakiwa wawili Dorcas Marwa na Maria Joseph wameachiwa kwa dhamana kufuatia maombi yaliyowasilishwa na wakili wa utetezi, Erick Mutta mbele ya Hakimu Mkazi, Stella Kiama.

Kabla ya kuachiwa, washtakiwa hao walitakiwa bondi ya maneno ya Sh 2 milioni, kuwasilisha nakala moja ya kitambulisho na barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Kuachiwa kwa washtakiwa hao wawili leo kumefanya idadi ya walioachiwa kufikia 78 huku Zumaridi na wafuasi wake wengine watano wakiendelea kusota rumande.

Chanzo: Mwananchi
 
Mfalume wetu bado wawajamuachia tu..daah acheni hizo..kanisa linamuhitaji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom