Upelelezi kesi ya waiba Konyagi bado

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Upelelezi kesi ya waiba Konyagi bado


na Mwandishi wetu


UPELELEZI wa kesi ya kuvunja na kuiba katika ghala la Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited, inayowakabili walinzi wa kampuni ya KK bado haujakamilika.
Mwendesha Mashtaka, Inspekta Nassoro Sisiwaya, aliiomba Mahamama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo kutokana na sababu hiyo.
Hakimu Flora Mushi anayesikiliza kesi hiyo, alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 27 mwaka huu, itakapotajwa tena.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Ezekiel John (22), Hamisi Mustapha (32) na James Shetta (21). Katika kesi hiyo, wanadaiwa kuvunja ghala la kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi), na kuiba katoni 232 za pombe aina ya konyagi.
Pia wanadaiwa kuiba mifuko ya plastiki 318 maarufu viroba iliyokuwa na konyagi ndani yake vyote vikiwa na thamani ya sh 36,186,042 mali ya kampuni hiyo
 
Kuna uhaja wa sheria za kuwazuia polisi kumkamata mtu na kumweka ndani zaidi ya massa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani .............vile vile sheria ya kukataza watuhumiwa kusota ndani zaidi ya miezi mitatu kabla ya kesi zao kusikilizwa..............Huu msamiati wa ushahidi haujakamilika umekuwa ni msumeno wa kutesa raia bila ya sababu.........kwa kifupi kama ushahidi haujakamilika sasa polisi walimkamataje raia?
 

Kesi zingine ni kukomoana tu, mlalamikaji yuko dar, wahasibu na wakaguzi wa mahesabu wako dar, kiwanda kiko dar na wapelelzi pia wako dar. Sioni sababu ni kwa nini upelelzi uchukue miezi miwili au mitatu.

Mahakimu wetu ni wagumu sana kutumia busara za kawaida kubaini kuwa hapa ni kukomoana, hasa ukizingatia kuwa sheria ya sasa inataka mtu adeposit nusu ya hela iliyoibiwa katika kesi hii ni shs 39millioni. Sheria ipo lakini kutokana na kuwa mahakimu wanashindwa kubaini kesi za uongo na ukweli wanakuwa wazito kutoa dhamana na au kufuta kesi.

Mwisho, vifungu vya dhamana inabidi viangaliwe na kurekebishwa vinafanya administration of justice kuwa mzigo mkubwa sana kwa serikali bila sababu yoyote.Matusi ndani bila dhamana, bangi weka ndani, wadada poa weka ndani, wapiga debe weka ndani. Kwa kila mtu mmoja anayekaa rumande mlipa kodi anagharamia dearly, so to speak.
 

KATIBA MPYA INAWEZA KUPUNGUZA HAYA MADUdU YA MAHAKAMA PIA
 
KATIBA MPYA INAWEZA KUPUNGUZA HAYA MADUdU YA MAHAKAMA PIA

Nafasi za mahakimu hazipo chini ya katiba, havyo kama hawa mahakimu watakuwepo bado hii ishu itakuwa vivi hivi. Sheria ya kuendesha kesi za jinai ibadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…