Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Upelelezi kesi ya waiba Konyagi bado
na Mwandishi wetu
UPELELEZI wa kesi ya kuvunja na kuiba katika ghala la Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited, inayowakabili walinzi wa kampuni ya KK bado haujakamilika.
Mwendesha Mashtaka, Inspekta Nassoro Sisiwaya, aliiomba Mahamama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo kutokana na sababu hiyo.
Hakimu Flora Mushi anayesikiliza kesi hiyo, alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 27 mwaka huu, itakapotajwa tena.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Ezekiel John (22), Hamisi Mustapha (32) na James Shetta (21). Katika kesi hiyo, wanadaiwa kuvunja ghala la kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi), na kuiba katoni 232 za pombe aina ya konyagi.
Pia wanadaiwa kuiba mifuko ya plastiki 318 maarufu viroba iliyokuwa na konyagi ndani yake vyote vikiwa na thamani ya sh 36,186,042 mali ya kampuni hiyo