Upelelezi kesi ya Zumaridi haujakamilika, kwanini anashikiliwa?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwenye himaya ya walamba asali uongo uongo ndiyo kwao. Mambo nyeti hufanyiwa siasa.

Alisema Samia watuhumiwa waache kukamatwa bila upelelezi kuwa umekamilika. Hizo kumbe zilikuwa hekaya za abunwasi tu.

Kumesikika Mwanza:

"Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hemedi Khalid ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Diana Bundala, maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’ haujakamilika."

Tabora Nako,

""Watu wasikamatwe kabla ya uchunguzi," Waziri Mkuu Majaliwa haimuhusu?"

Uongo uongo tu kwenye mambo nyeti. Huu ni muendelezo ule ue wa kutuona wananchi ni kama mang'ombe tu, kwa kutopigania kuona haki zetu zinalindwa kwa mujibu wa katiba.

Yapi yameheshimiwa? Ni kuacha kupigwa au kuteswa watuhumiwa? Ni polisi traffic kujazana mabarabarani kufukuzia rushwa? Ni takukuru kuwajibika? Ni maoni ya wananchi kuheshimiwa? Nk, nk?

Ama kwa hakika, "watanzania tatizo letu ni ujinga uliopitiliza." -- FAM.
 
Nimeshangazwa sana na hii habari, mtuhumiwa anashikiliwa gerezani zaidi ya miezi 7 lakini kila siku upande wa mashtaka wanadai upelelezi haujakamilika, sasa kwanini walimkamata?

Inavyoonekana, mashtaka wanayomtuhumu nayo yenye uzito ni yale ya kuwafanyia fujo polisi siku waliyoenda kumkamata, kinyume na hapo hakuna mashtaka mengine ya maana waliyonayo, ndio maana kila siku upelelezi bado haujakamilika.

Haya mambo yanaonesha tulivyo na mfumo mbovu wa kimahakama, ajabu hakimu anatakiwa kuwapa upande wa mashtaka angalizo, kesi ikiitwa tena mahakamani upelelezi ukiwa bado haujakamilika mshtakiwa aachiwe huru.
 
Haki zetu zinapaswa kuwa wazi kwenye katiba wala si kuyategemea maneno yao matupu majukwaani.
 
Nimepita Leo kwenye eneo ambalo huyu mama alikuwa anakaa na kufanya shughuli zake nilisikitika Sana kuona mazingira yalivyo .

Jeshi la police ni jeshi lenye vilaza nje na kupiga watu hawana maarifa yoyote ya kupata taarifa toka kwa mtuhumiwa na mbaya zaidi mahakama zetu zimekuwa za hovyo Kama bank za Tanzania zilivyo na wizi wa pesa za watu.
 
Kwenye himaya ya walamba asali uongo uongo ndiyo kwao. Mambo nyeti hufanyiwa siasa.

Alisema Samia watuhumiwa waache kukamatwa bila upelelezi kuwa umekamilika. Hizo kumbe zilikuwa hekaya za abunwasi tu.

Kumesikika Mwanza:

"Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hemedi Khalid ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Diana Bundala, maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’ haujakamilika."

Tabora Nako,

""Watu wasikamatwe kabla ya uchunguzi," Waziri Mkuu Majaliwa haimuhusu?"

Uongo uongo tu kwenye mambo nyeti. Huu ni muendelezo ule ue wa kutuona wananchi ni kama mang'ombe tu, kwa kutopigania kuona haki zetu zinalindwa kwa mujibu wa katiba.

Yapi yameheshimiwa? Ni kuacha kupigwa au kuteswa watuhumiwa? Ni polisi traffic kujazana mabarabarani kufukuzia rushwa? Ni takukuru kuwajibika? Ni maoni ya wananchi kuheshimiwa? Nk, nk?

Ama kwa hakika, "watanzania tatizo letu ni ujinga uliopitiliza." -- FAM.
Kama zumaridi hakuwa na kadi ya chama hai atateseka sana.
 
Hapa ndipo lilipo tatizo letu watanzania. Wenye hata nia tu ya kuongelea haki za Zumaridi hawapo.

Mentality za kijinga -- FAM, kwamba kavuna janga atakula na wa kwao.

Haki inapaswa kuonekana kama haki iliyokiukwa bila kujali mwathirika ni nani.
 
Nimepita Leo kwenye eneo ambalo huyu mama alikuwa anakaa na kufanya shughuli zake nilisikitika Sana kuona mazingira yalivyo .

Jeshi la police ni jeshi lenye vilaza nje na kupiga watu hawana maarifa yoyote ya kupata taarifa toka kwa mtuhumiwa na mbaya zaidi mahakama zetu zimekiwa za hovyo Kama bank za Tanzania zilivyo na wizi wa pesa za watu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Tunapaswa kupaza sauti kuidai haki ya Zumaridi na wenzake inayokiukwa kwa makusudi na jeshi la polisi. Leo kwake kesho kwa mwingine
 
Nimeshangazwa sana na hii habari, mtuhumiwa anashikiliwa gerezani zaidi ya miezi 7 lakini kila siku upande wa mashtaka wanadai upelelezi haujakamilika, sasa kwanini walimkamata?

Inavyoonekana, mashtaka wanayomtuhumu nayo yenye uzito ni yale ya kuwafanyia fujo polisi siku waliyoenda kumkamata, kinyume na hapo hakuna mashtaka mengine ya maana waliyonayo, ndio maana kila siku upelelezi bado haujakamilika.

Haya mambo yanaonesha tulivyo na mfumo mbovu wa kimahakama, ajabu hakimu anatakiwa kuwapa upande wa mashtaka angalizo, kesi ikiitwa tena mahakamani upelelezi ukiwa bado haujakamilika mshtakiwa aachiwe huru.
Kama hizo ndio tuhuma,

Clip zipo sote tumeziona.

Kuna haja ya kuwa na upelelezi zaidi??
 
Kwa kifupi huyo Zumaridi wala hana kesi kubwa sana kiasi kwamba inaweza kumkalisha gerezani mda huo, shida kubwa ni kwamba kuna watu wa system aliwatukana na kuwajibu jeuri na mmoja wapo alimtaja hadi jina sasa sijui alisahau huyo mtu aliwahi kuwa General wa Jwtz na RSO pia ila now ni mchungaji so kazi anayo labda akaombe msamaha
 
Kwamba si kwa mujibu wa sheria ila ni personal vendetta? Hii mbona ni Tanzania tu? Mbona mtoto wa yangachawene anadunda mitaani? Yeye hakutukana?
 
Hizi hadithi za watu wasikamatwe kabla ya upelelezi ni uongo wa mchana.... polisi Tanzania hawawezi kufanya hivyo!
Rais haoni kuwa hatoshi kwa kusimama majukwaani kupiga hadithi za sungura na fisi kwenye haki zetu? Kwa hakika tunahitaji katiba itakayotusimamia. Siyo hawa ndumila kuwili!
 
Back
Top Bottom