Upelelezi kesi ya Zumaridi haujakamilika, kwanini anashikiliwa?

Kwamba si kwa mujibu wa sheria ila ni personal vendetta? Hii mbona ni Tanzania tu? Mbona moto wa yangachawene anadunda mitaani? Yeye hakutukana?
Mkuu huyo yangawene alitukana dagaa wa ziwa nyasa wala hawana madhara kabisaa, ila huyu alienda kuvua Sangara ziwa victoria na Sindiria unategemea nini🤣🤣🤣
 
That's too personal, katukanwa Yeye binafsi, amfungulie kesi kuliko kumshikilia
 
Mkuu huyo yangawene alitukana dagaa wa ziwa nyasa wala hawana madhara kabisaa, ila huyu alienda kuvua Sangara ziwa victoria na Sindiria unategemea nini🤣🤣🤣

Hakuna aliye na haki ya kuchukua sheria mkononi au hata kumkomoa yeyote akitumia jina la JMT.

Kama ndivyo anavyofanyiwa raia huyu wahusika hawastahili kushikilia nyadhifa za umma.

Mambo kama haya lazima kukazia kwenye katiba mpya ambayo kwa hakika haiwezi kusubiri tena.

Tunaishi kwa kudra za watu? Haiwezekaniki!
 
Kuna walioko huko miaka 7
 

Kwa hiyo anajejiita Mungu kafungwa na mamlaka za duniani?
 
Katiba lenyewe ndio hili mkuu alituachia mzee mchonga unategemea nini hapa mpaka tupate kitabu kipya
 
Hakika ni uonevu Mkubwa kabisa juu ya huyu mama. Anazo mali zisizo hamishika si wamuachie akachunge kondoo zake upelelezi ukikamilika si anapatikana. Kesho ameshinda kesi nani atamlipa mda wake Kwann tunakuwa primitives kiasi hiki. Ulimwengu wa SAsa hata ukiachwa huru huwezi jificha utapatikana tu hasa kwa mtu maarufu kama huyu.
Serikali za kiafrica mambo ya maana huwa haidili nayo.
 
Mimi ni nani hata nidai haki ya mungu mtu chini ya jua? Ni wakati wa mungu mtu chini ya jua kuonesha uungu wake
Hapa ndipo ulipo ujinga wetu -- FAM

Kwamba Kila tunayemdhania ni mchuma janga na akale na wa kwao.

Kwani mkuu wewe ni mlamba asali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…