Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kesi ya mauaji inayowakabili viongozi watano wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kilolo, imeahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.
Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Sauli Makori, leo Jumanne, Januari 21, 2025, ameieleza Mahakama kuwa bado kuna mashahidi muhimu na vielelezo vinavyohitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Hivyo, ameiomba Mahakama iahirishe kesi na ipange tarehe nyingine ya kutajwa.
Soma Pia: Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana
Hakimu Mayagilo hakupinga ombi hilo na kuahirisha kesi kwa siku 14 huku akisema itatajwa tena Februari 4, 2025.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Kilolo, Hedikosi Kimwaga, Diwani wa Nyanzwa, Boniface Ugwale, Katibu wa Mbunge wa Kilolo, Kefa Walles, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mlandege, Wille Chikweo na Silla Kimwaga.
Wanakabiliwa na kesi ya mauaji wakituhumiwa kumuua aliyekuwa Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kilolo, Christina Kibiki (56).