Upendo Furaha Peneza: Gold in the rough. Vijana CHADEMA mpo?

Upendo Furaha Peneza: Gold in the rough. Vijana CHADEMA mpo?

sweya lugendo

Member
Joined
Dec 7, 2013
Posts
56
Reaction score
22
Mara ya kwanza kumwona na kumsikiliza live ilikuwa Kakola Kahama,mara ya pili juzi Nyang'hwale,nimemsoma akiwa Uganda na aliyekuwa kiongozi mathubuti wa chama pinzani Besigye na kwenye mijadala kadhaa ya gesi akitokea Norway.

Ni kijana binti mdogo mwenye uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja za kitaifa na kimataifa,huwezi kumsikiliza usimpongeze vinginevyo uwe na wivu uliopitiliza mno.

Naomba achukue fomu ya uongozi wa juu kabisa wa Bavicha taifa na asiogope vitisho na mbwembwe za wengine, vijana wenzake wamuunge mkono maana kakamilika.

Nawasilisha kama kuna mwenye kumfahamu zaidi amwagike.
 
Dada anasitahili nafasi yoyote ndani na nje ya chama huyo,nilimfuatilia maisha plus vizuri pia
 
Sina hofu na chadema,ni chama pekee ambako vijana wanathamiwa sana bila shaka watamwona japo mamluki nao wanavizia vizia
 
Kama ndo yule wa maisha plus basi uraia wake una utata utakuja kumsumbua mbeleni. Kwa kifupi ni mnyarwanda kama huamini fuatilia post zake nyingi fb.
 
Eti, Kisa mtu kashiriki Maisha Plus...Mnataka awe M/Kiti wa Bavicha??? Jamani hebu kuweni makini vijana wenzangu.
No mkuu, suala sio ushiriki wake maisha plus bali ni je ana uwezo?kiongozi anaweza kutokea mahala popote.
 
Fomu zipo wazi kila mwenye sifa na kamanda wa kweli asiye na element za uchumia tumbo anakaribishwa na ni haki yake kutuongoza sisi vijana wenzake kupitia CDM!
 
Kiongozi suala la uzalendo kwa bahati mbaya halipimiki kirahisi,naamini chadema wana mfumo thabiti wa kusaili Wagombea wao

OK, let's wait and see, mkuu.
Tho am deep fear wit her inborn character.
 
Tusiogope vijana au viongozi wapya kuingia kwenye chama kwa hofu kubwa ya mamluki.Najuwa tahadhari kubwa inatakiwa,kumbukeni Marekani bila kufungua Milango kwa wahamiaji isingekuwa hapo ilipo
 
Back
Top Bottom