Upendo Kilahiro afunga ndoa ya pili

Upendo Kilahiro afunga ndoa ya pili

“PORNEA” SABABU YA KUMWACHIA MKE

Tunaendelea. Acha tung’oe nanga tena. Vijana, kati ya maswali yenu mliyoniomba niwafafanulie ni sababu ya kumwacha mke iliyotajwa katika Mt 19:9. Mliniandikia na kuniuliza ifuatavyo: “Baba twaomba tuulize, mbona kwenye Injili Yesu anaruhusu talaka kama kuna uasherati umetokea kwenye ndoa wakati mafundisho ya Kanisa Katoliki hayaruhusu hivyo?”

Hivi ndivyo mlivyoniwekea. Kwa kweli, mimi sijui msingi wa swali lenu kama ni hamu ya kutalikiana au kutaka kujua tu. Lakini kwa vyovyote sina sababu ya kuchimba mahali pakavu kama hapo. Mimi naenda kwenye swali lenu tu.

Muktadha wa Swali la Mafarisayo
Awali ya yote, acheni niwapeni muktadha wa swali aliloulizwa Yesu. Ni hivi katika Kum 24:1-4 imeandikwa hivi: “Ikiwa mwanaume ameoa mke na baadaye akawa hapendezwi naye KWA SABABU AMEONA KWAKE KITU KISICHOFAA, basi huyo mwanaume akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, kisha huyo mwanamke akaondoka, akaolewa na mwanaume mwingine, kama huyo mume wa pili akimchukua, akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, au kama huyo mumewe akifa, basi, yule mume wa kwanza haruhusiwi tena kumchukua huyo mwanamke kuwa mke wake kwa sababu alikwisha kutiwa najisi. Kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu Mwenyezi.”

Marabbi Wawili
Nukuu hii ndiyo iliyo nyuma ya swali la Mafarisayo waliokuja kumtega Yesu kwa swali juu ya talaka. Kifungu hiki kilishakuwa “habari ya mjini” kati duru za kisomi za Wayahudi na matokeo yake marabbi (walimu) wawili maarufu walijikuta wakipingana katika maelezo ya hicho “KITU KISICHOFAA” (kwa Kiebrania “ERWAT DAVAR”) ambacho mwanaume akikiona kwa mkewe kinaweza kuwa sababu ya kumwandikia na kumpa talaka. Marabbi hao walikuwa Hillel na Shammai. Sasa yasikilize mafundisho yao.

Haki ya kuacha ilikuwa ya mwanaume siyo mwanamke. Mume ndiye aliyeacha, mke ndiye aliyeachwa. Rabbi Hillel, babu yake Gamalieli aliyekuwa mwalimu wa Mtume Paulo, alisema “KITU KISICHOFAA” (“ERWAT DAVAR”) ni kitu chochote kile kingalichoondokea kutompendeza mume, mathalani, mke kuwa mchafu, kuacha kumwamkia, kuvaa vibaya na kadhalika na hata kama mwanaume angemwona mwanamke mwingine mwenye sura nzuri aliyetaka amwoe badala ya huyo aliyemwoa na kumwona ana sura mbaya.

Lakini kinyume cha Rabbi Hillel alisimama Rabbi Shammai ambaye alisema “KITU KISICHOFAA” (“ERWAT DAVAR”) kinachoweza kutumika kama sababu ya mume kumwacha mkewe sharti kiwe kitu chenye uzito wa kutosha, kwa mfano, ugoni, kutembea uchi mbele ya watu au kitu kingine cha aina hiyo kingalichofanya uchi wa mwanamke uonekane.

Pande hizi mbili zilikinzana sana na, kwa bahati njema au mbaya, kila upande ulikuwa na wafuasi wengi. Ndiyo katika muktadha wa mjadala mkali juu ya “KITU KISICHOFAA” (“ERWAT DAVAR”) wanapokuja Mafarisayo kumjaribu Yesu kama anajua kitu ama yeye naye ni maamuma tu. Basi, ndipo walimuuliza kama ni halali kumwacha mke kwa sababu yoyote, yaani kama alivyokuwa akifundisha Rabbi Hillel au la.
Kumbe, Yesu alitumia fursa ya swali lao, kuwasahihisha akina Hillel na Shammai japo pasipo kuwataja kwa majina. Kwa jibu lake aliwaponda marabbi wote wawili kwa kufundisha kitu kisicho matashi ya Mungu. Badala ya misimamo yao ya kuruhusu talaka akawafundisha wanadamu wote kwamba talaka ni kitu haramu kwa maana hutenganisha alichounganisha Mungu tangu mwanzo.

Yesu Alitaja “Pornea”
Hata hivyo, katika maelezo yake Yesu alisema kinachoweza kuwatenganisha watu ni ‘PORNEA’. Lakini kwa kutaja sababu hiyo swali likatuzukia wanadamu wa leo kuulizana hiyo “PORNEA” ni nini. Kumbe, hapa ndipo watafsiri wetu wanapopwelea kwa kushindwa kutafsiri kisahihi neno hilo. Ndipo katika Kiswahili walipotafsiri kwa mkato “uasherati” au “uzinzi.”

Huu ni mkasa wa kitaaluma. Najua watafsiri wengine walichungulia tafsiri za Kiingereza “fornication” au “adultery” ndipo wakatutafsiria “PORNEA” kwa maneno ya “uasherati” au “uzinzi” na hivi nao wao kulistawisha tatizo lile lile la tafsiri. Je, mnanielewa hadi hapa? Kama ndivyo, tusonge mbele pamoja. Ikiwa sijaeleweka hapo, rudia walau mara moja kusudi jibu langu lisikubabaishe huko mbele ya safari.
Vijana, kumbe hapo ndipo tulipofikia, yaani kwenye tatizo la kutafsiri kwa usahihi neno “PORNEA” katika Mt 19:9. Mahali pengi husomwa tafsiri ifuatayo: “Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini, naye amwoaye yule aliyeachwa azini.” Lakini kuna tafsiri nyingine inayosomeka neno “uzinzi” mahali pa neno “uasherati”.

Kwa vyovyote, tofauti hii si kitu cha msingi, mamoja iwe “uasherati” au “uzinzi”, maneno yote mawili ni tafsiri nyepesi mno ya neno lenye maana nzito zaidi - “PORNEA”. Maneno yote hayo mawili yanapwaya kabisa, wala hayakidhi haja ya tafsiri makini. Alichosema Yesu ni kizito zaidi. Hivi hapo “uasherati” au “uzinzi” isieleweke kama uasherati wa kawaida au uzinzi wa kawaida isipokuwa uhusiano wa kindoa kati ya watu waliokaribiana kidamu. Yaani uhusiano wa mahirimu au maharimu.

Uhusiano wa aina hii ndiyo sababu ya kuwatawanyisha watu waliothubutu kuoana. Ndiyo kisa Kanisa Katoliki hukataa kuwafungisha ndoa watu waliokaribiana kidamu. Watu waliokaribiana kidamu hadi digrii ya nne marufuku kuoanishwa katika Kanisa Katoliki. Nia ya kufunga ndoa inapotangazwa mara tatu ni pamoja na kutoa fursa kwa watu wanaowajua wanandoa watarajiwa kama wamekaribiana kidamu watoe taarifa mahali panapohusika.

Kukataa kuwafungisha ndoa mahirimu au maharimu siyo tu kutii kauli ya Yesu Kristo bali pia ni kujiepusha na madhara ya kukaribiana kidamu wazazi. Yaani kama mifugo ya sungura, nguruwe na bata inavyodhurika kwa damu zilizokaribiana za wazazi wao vivyo wanadamu. Watoto wa wazazi waliokaribiana damu si mara haba kuzaliwa na vilema vya kurithi kwa vinasaba pamoja na mikasa ya kuzaliwa na vilema vya upofu, uziwi na ububu.

Waulize madaktari wakupe vinaganaga vya kwa nini hutokea hivyo na kisha uende Israeli wanakong’ang’ania kuoana wao kwa wao ushuhudie kwa macho vilema vya sampuli hii vilivyotamalaki. Basi, mkasa huu ukusaidie kuelewa kwa nini Yesu alipokuja duniani katika umbo la mwanadamu aliwashuhudia jamaa zake Waisraeli wakirabiwa na vilema lukuki (Lk 4:18, 7:22).

“Pornea” na “Moicheia”
Namalizia kwa kusema “PORNEA” si “MOICHEIA”. “MOCHEAIA” ndiyo uasherati au uzinzi tunaoufahamu (rej. Yn 8:3-4). Jambo hili tumeliangalia vizuri na kutafsiri vyema katika Biblia ya Kiafrika. Narudia kusudi kushadidia jibu langu. Neno la Kigiriki lililotumika ni “PORNEA” wala si “MOICHEIA”. Sheria ya Kanisa namba 1151- 1152 zina kitu cha kutuambia Wakatoliki. Zitafute uzisome.
Uasherati na Uzinzi Kusameheana kwa Kanuni ya Dhahabu
Katika Kanisa Katoliki, uasherati kama uasherati au uzinzi kama uzinzi si sababu ya kumwachia mke isipokuwa kutenganishwa kwa muda wa walau miezi sita tu. Baada ya kupoa hasira na kusameheana ndani ya miezi sita, wanandoa hualikwa kurejeana kusudi waendelee kuishi kama mume na mke. Kushikana ugoni huwa ni kuvunjika kwa koleo tu yaani kusikokuwa mwisho wa uhunzi. Ngumu lakini ndivyo inavyopasa kufanyika.

Dawa ya mgogoro wa uasherati na uzinzi ni msamaha kwa kanuni ya dhahabu. Kanuni ya dhahabu (Mt 7:12) inasema, Mtendee mwenzako unavyopenda utendewe mwenyewe, na katika maisha ya ndoa hakuna anayependa aachwe kwa sababu amekosa uaminifu. Hivyo, isiwe kwa kuwa umekosewa wewe mwenzio afunge virago aende zake wakati ukikosa mwenyewe eti mwenzio akusamehe! Basi, kusudi msamaha usiwe wa upande mmoja haki yake ni WOTE KUSAMEHEANA. Kwa herini tena!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
 
Hata uasherati hauvunji ndoa ni misinterpretation tu. Yesu anasema toka mwanzo halikuwa kusudio la Mungu kuwe na talaka lakini Musa aliruhusu sababu ya ugumu wa mioyo ya wana wa Israel.

Lile neno ambalo Yesu anaposema alichounganisha Mungu mwanadamu asitenganishe alafu aruhusu talaka? Lile andiko wanalochukua wengi la "isipokuwa uasherati" linatafsiriwa vibaya. Kwanza kwa wataalam wa Bible wanasema neno uasherati lilitumika kwa kukosa msamiati sahihi lakini kutoka kwenye lugha halisi si uasherati. Nitatafuta ufafanuzi wa kina niweke hapa.

Kwa hiyo kwa MTAZAMO wako mkuu watu wote wanaotafsiri kwamba ndoa inatenganishwa na kifo au uasherati wanatupiga fix?
 
Jaman wakristo ndoa si ni moja tu inakuwaje mnaoa na kuolewa tena? Na nyie viongozi wa dini ya kikristo inakuwaje mnafungisha ndoa ya namna hii?
 
Siwezi kuendelea kuishi katika ndoa ya mateso kwa kunung'unika eti kisa kuogopa hukumu za walimwengu, nyie hukumuni ila ndo kashaolewa, wengine humu wanamuonea wivu tu muonekano wake na uhaba wa waoaji ila ndo kaolewa 2 times Tena kwa heshima zote, wewe uko chura km beseni hata posa ya uchumba hujawahi kushuhudia😂😂😂lazima ujibanze kwenye biblia inasema🤣🤣🤣🤣
 
Siwezi kuendelea kuishi katika ndoa ya mateso kwa kunung'unika eti kisa kuogopa hukumu za walimwengu, nyie hukumuni ila ndo kashaolewa, wengine humu wanamuonea wivu tu muonekano wake na uhaba wa waoaji ila ndo kaolewa 2 times Tena kwa heshima zote, wewe uko chura km beseni hata posa ya uchumba hujawahi kushuhudia[emoji23][emoji23][emoji23]lazima ujibanze kwenye biblia inasema[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Watu hawajui ni nini kilimtoa kwa ndoa ya kwanza. Mambo ya ndoani ni mazito mno. Kama kapata furaha nyingine tumuwache
 
Back
Top Bottom