Upendo wa Trump kwa Putin ni wa ajabu sana

Upendo wa Trump kwa Putin ni wa ajabu sana

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Muda mfupi uliopita, Donald Trump alizungumza kwenye Fox News, akitoa maoni yake kwa mara ya kwanza tangu rais wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana katika Ikulu ya White house Jumatatu, pamoja na washirika wengine wa Ulaya.

Trump anasema anapanga mkutano kati ya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin na Zelensky ambao hautamjumuisha hapo awali.

"Ikiwa hiyo itafanikiwa, basi nitakwenda na kuufunga," anasema.

Anasema anatumai Zelensky "ataonesha kubadilika" katika mazungumzo.

Trump anasisitiza kuwa wanajeshi wa Marekani hawatakuwa Ukraine kama sehemu ya dhamana ya usalama inayotafutwa na Kyiv.

Mataifa ya Ulaya kwa upande mwingine yanaweza kuwa na wanajeshi nchini Ukraine kama sehemu ya makubaliano, Trump anasema.

Pia anasema washirika wa Ukraine na Nato wanapaswa kuachana na juhudi za kuifanya Ukraine ijiunge na muungano wa usalama na kurejesha Crimea, ambayo Urusi iliikalia mwaka 2014.

"Mambo yote mawili hayawezekani," anasema.

Anasema mazungumzo yake na Putin jana haikufanyika mbele ya washirika wa Ulaya na Nato. "Nilidhani hiyo itakuwa ni dharau kwa Rais Putin," anasema.
 
Tangazo la AMANI NA USALAMA LIPO KARIBU SANA....Huo ndo utakuwa mwanzo wa DHIKI KUU(The great tribulation) lililotajwa na Yesu.....

Mwisho uko karibu sana.... Mtafute Mungu kabla ingawa bado anapatikana.
 
Unajua ni amani gani inazungumziwa kwenye maandiko?
 
Unajua ni amani gani inazungumziwa kwenye maandiko?
Amani ya kwamba vita na migogoro baina ya nchi na nchi itakuwa imepatikana, umoja umepatikana 1 thessalonians 5:1-3

Ikiwa kuna zaidi ningependa kufahamishwa... ahsante..
 
Ukifatilia ya uchambuzi wa mitandao na jinsi jamaa wanavo pendana inshangaza sana ama kweli ukitaka ishi vizuri. Epuka mtu masikinisana, mtu mwenye ndotokubwa,na mwanasiasa

Fullstop,kwishaaaa
 
Trump anawaambia wanachama wenzake wa NATO ukweli ambao wanaujua ila hawataki kukiri!... Tangu lini mbwa akaweza kuchukua kitoweo mdomoni mwa simba?

Hatima ya Ukraine haiamuliwi na yeyote isipokua Urusi pekee! Trump alitaka kuwaambia wenzake kwamba, sisi NATO tutake au tusitake ni lazima tukubaliane na masharti ya Urusi
 
Nifahamishe tafadhali....
Okay, vita vinavyozungumzwa kwenye maandiko, ni 'spiritual war' au religion war.iko hivi, kutakuwa na muungano wa kidini kwa mgongo wa Baba wa imani , Abraham, muungano ambao utasifiwa na wanadamu kwa kuwa hapatakuwepo na ubaguzi,( hapo watu watasema , "TUMEPATA AMANI" kumbe ndio maangamio yamewafika. Muungano huu utakuwa na agenda iliyojificha ambayo ni.
1. Kumshudia ibilisi/ shetani pasipokujua.
2. Kuuwa " to elimination " au kuwatesa wakristo wa kweli kwa njia ya kutunga sheria kali, moja wapo ni hii ya ugaidi, sheria za kiuchumi, yaani kununua na kuuza kwa masharti ya kutii sheria za kitaifa au kimataifa. Sheria hizi zitakuwa zinampinga Mungu wa mbinguni.
 
Hivi labda mimi sielewi vyema UN huwa ni wa matamko tu? bila kuwa na juhudi za kusimamisha mapigano Duniani? Maana utasikia kumepigwa kura ya kulaani mauaji mahala fula halafu basi kimyaaa, mpka unasikia mara Raisi wa Nchi flani kaitisha mkutano wa kuwapatanisha sasa hapo ndipo napo jiuliza UN ni yamatamko tu?
 
Amani ya kwamba vita na migogoro baina ya nchi na nchi itakuwa imepatikana, umoja umepatikana 1 thessalonians 5:1-3

Ikiwa kuna zaidi ningependa kufahamishwa... ahsante..
1 Kuhusu nyakati na matukio yasiyo wazi, ndugu, hamna haja ya kuwa na wasiwasi sana.

Ushaambiwa usiwe na wasi wasi sana, ila nashangaa wewe una wasi wasi sanaaaa😂

Hiyo siku hakuna aijuaye
 
Okay, vita vinavyozungumzwa kwenye maandiko, ni 'spiritual war' au religion war.iko hivi, kutakuwa na muungano wa kidini kwa mgongo wa Baba wa imani , Abraham, muungano ambao utasifiwa na wanadamu kwa kuwa hapatakuwepo na ubaguzi,( hapo watu watasema , "TUMEPATA AMANI" kumbe ndio maangamio yamewafika. Muungano huu utakuwa na agenda iliyojificha ambayo ni.
1. Kumshudia ibilisi/ shetani pasipokujua.
2. Kuuwa " to elimination " au kuwatesa wakristo wa kweli kwa njia ya kutunga sheria kali, moja wapo ni hii ya ugaidi, sheria za kiuchumi, yaani kununua na kuuza kwa masharti ya kutii sheria za kitaifa au kimataifa. Sheria hizi zitakuwa zinampinga Mungu wa mbinguni.
Sheria za kiuchumi zinampingaje Mungu?
 
Hivi labda mimi sielewi vyema UN huwa ni wa matamko tu? bila kuwa na juhudi za kusimamisha mapigano Duniani? Maana utasikia kumepigwa kura ya kulaani mauaji mahala fula halafu basi kimyaaa, mpka unasikia mara Raisi wa Nchi flani kaitisha mkutano wa kuwapatanisha sasa hapo ndipo napo jiuliza UN ni yamatamko tu?
Kazi ya U.N ilishaisha kwa sasa hivi ni geresha tu, ndio maana Trump huwa hataki kuchangia ama kusaidia mashirika ya U.N

U.N ilianzishwa na USA kwa minajili ya kufuta ukoloni ili atawale dunia vizuri ndivyo ninavyoamini mimi
 
Sheria za kiuchumi zinampingaje Mungu?
Ume quote kifungu cha biblia, imenipa imani kwamba ww ni msomaji mzuri wa maandiko, naamini umesoma kitabu cha ufunuo wa yohana kuuza na kununua bila kuwa na chapa ya mnyama. Ndio namaanisha. Kuhusu uchumi.
 
Back
Top Bottom