SnowBall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 3,052
- 2,842
Wanajamvi salaam!
Ni kawaida sana kwa wanawake walioko kwenye NDOA kuwa na mapenzi makubwa na watoto wao. Wengine hudai kibaolojia urafiki wa mama na mtoto uko 'strongly linked' kuliko ule wa baba..husema wamama wana stake kubwa sana kwa watoto kuanzia mimba, ulezi na pengine hata ukuaji wa watoto wenyewe...Lakini hii pia haiondoi dhana ya uwepo wa mama wakatili kwa watoto. Mfano tumeona wanawake wengi tu wakitupa watoto wao wa kuzaa wenyewe majalalani au pia wanawake kutesa watoto wao wa kambo. Kiufupi yote yanawezekana..i mean mwanamke kuwa mkatili au mpole katika nature yake.
Kutokana na jamii kuwa na mentality ya namna hii ndio maana tunasikia 'slogan' kama 'hakuna kama mama' na nyingine zinazofanana na hizo. Lakini hali ikiwa hivyo kwa kina mama sidhani pia kama ni sahihi kusema wababa hawana mapenzi kwa watoto wao as walivyo wamama..Manake pia tunaona katika baadhi ya familia watoto wakiwa wanawapenda wababa zao kuliko pengine mama zao..Vyovyote iwavyo inawezekana katika mazingira flani upendo wa baba ukawa mkubwa kwa watoto kuliko wa mama au saa zingine kinyume chake.
Lakini hali ikiwa hvi ni mara nyingi utasikia kwenye mahusiano yanayolegalega wanawake wakisema 'Yaani naishi naye kwa ajili ya watoto tu'?..It means upendo unakuwa umekufa ila kwa vile kuna watoto wamama wanakuwa wanaishi na wenzi wao alimradi tu siku ziende..It means wapo tayari ku'sacrife' anything kwa ajili ya watoto. Kwa wababa ni nadra kusikia hili..pengine nalo lipo hapa sina uhakika sana..
Hebu sasa niwaulize wamama/wababa kama mko tayari kuishi na wenzi wenu kwa maisha ya kuungaunga yasiyo na furaha kisa mnalea watoto...JE? KWA NINI MNASHINDWA KULEA WATOTO WA KAMBO???..Au nyie ni wabinafsi na wanafiki tu kwa watoto mliowazaa wenyewe???..Kumbukeni uchungu uliokushika wewe ndio uliomshika mwanamke mwenzio!!!Ukiwa na upendo kwa watoto kwa nini ubague labda tujiulize upendo wa mama kwa watoto ni wa kinafiki???
Nawasilisha!