Upgrading from Toyota ist to AUDI A4

Pamoja ila usiombe ushauri kwa watu wa Toyota hawanaga clue.....zungumza na wamiliki.

Pia usinunue magari ya miaka ya zamani sijui 2002 3 4 huko...


Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Nami nilitaka kumwambia juu ya miaka. Tena anunue kuanzia gari za 2010. Kama nakumbuka sahihi hizi European cars zilipitia mabadiliko makubwa katika emissions na performance kutokana na matakwa ya kimiongozo ya Umoja wa Ulaya. Hivyo gari ziliboreshwa zaidi ili kukidhi miongozo hiyo.
 
Yah...mimi BINAFSI naprefer kuanzia 2013 kama akiweza Europeam cars zilifanyiwa 'facelift' mwaka huo.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Huko unaenda kuootea ndugu yangu, hiyo audi ikikutana na masika ika savaivu basi jua unabahati sana🤣
 
Audi ni bora ukinunua mpya pamoja na binamu zake wa kijerumani ambao ni Benz na BMW. Kama huwezi nunua mpya basi komaa na Toyota, Honda,Kia to Hyundai ambazo reliability ni msingi wa biashara zao.
 
Kwamba ni za udongo zikinyeshewa zinamong'onyoka?
Acha aipitishe kwenye madimbwi halafu dashboard ikiwaka aipotezee kidogo kama alivyozoea kwenye Toyota.

Gari za mjerumani ni pasua kichwa kwa wamiliki wengi bongo kama huna ujuzi mwenyewe na unaenda kwa mazoea, kuna jamaa betri ya benz ndogo tu w204 ilikata moto akaamua kubusti akaua SAM(signal acquisition module) gari ilikuwa haiwaki na dashboard yote ilikuwa inamulika kama mti wa Christmas, na hapo mpaka kaja kujua tatizo diagnosis ilibidi aende CFAO Motors kipindi hicho ilikuwa 2014 w204 zinatafutwa kwa manati mafundi walikuwa wanalikimbia hawajui tatizo ni nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…