Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria pindi gari (hususan daladala) inapoanza kurudi nyuma baada ya kushindwa kupanda mlima? Yaliwahi kukukuta?

Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria pindi gari (hususan daladala) inapoanza kurudi nyuma baada ya kushindwa kupanda mlima? Yaliwahi kukukuta?

Hiyo ni ajali, kwenye ajali hakuna jibu la moja kwa moja, zaidi inategemea mazingira ya ajali.
Kama dereva angeweza angalau kulizuia, Yaani lisimame na kutokurudi nyuma, pengine ingekuwa salama kwa abiria wote kutoka.
Okay...
 
Tukio hili, walioruka walipona, nina mfano ambapo kulitokea ajali aliyeruka ni mmoja tu na ilitokea ndio namfahamu, na yeye pekee ndie aliyepoteza maisha kwa kiangukiwa na basi.
Daaah, changamoto sana mkuu ukizingatia daladala za hapa Tanzania ambazo 96% hazina seat belts.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria pindi gari (hususan daladala) inapoanza kurudi nyuma baada ya kushindwa kupanda mlima?

View attachment 1607527

Je, ulishawahi kujikuta katika hali hii na ulifanya nini?

Nimeamua kuomba ushauri hapa kwa maana kwamba siku ya tarehe 13 October 2020, ambapo mvua kubwa sana ilinyesha sana, nilipokuwa ninatoka Kitunda huku Dar sasa ninarudi Kivule nikiwa katika bodaboda maeneo ya sehemu moja wanaitwa kwa Mwailafu nilishihudia gari ya abiria almaarufu kama daladala ikirudi "reverse" baada ya kushindwa kupamba mlima mdogo kutokana na udongo wake kuwa unatereza kwa kiingereza wanasema "treacherous"

Katika harakati za kutaka kuokoa maisha yao kuna abiria wawili ambao ni wakaka wao wakaruka nje lakini abiria wengine wote wakabaki ndani ya daladala ile huku wakipiga mayowe wasijue nini la kufanya.

Mungu si Athumani, dereva wa ile gari alikuwa jasiri na shupavu alifanikiwa kuigonesha ile gari pembezoni mwa ukingo wa barabara hivyo kuzuia gari ile isiingie katika daraja kubwa ambalo bado linaendelea na ujenzi.

NB: Picha hapo juu haina uhusiano wowote na hicho kisa nilichosimulia.

Kuna baadhi ya watu wanadai kuruka wakati daladala/gari ime-fail brake mlimani sio uamuzi sahihi ila kuna baadhi wanadai kuwa ndio jambo jema la kufanya wakati wa janga la namna ile

Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria? Je, ulishawahi kujikuta katika hali hii na ulifanya nini?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Lengo ni kuokoa uhai so uamuzi wowote ni sahihi
 
Mimi kilinikuta HV

1. Tulikua kwenye bajaji tunaelekea huko mashambani..tulikua abiria watatu..mm nilikua nmekaa upande wa kushoto au mlangoni huku kwa abiria( kwa wanaopandaga bajaji watakua wameelewa)
2. Tukafika kwenye kimlima fulani hv..Dereva akakomaaa weee mwisho bajaji ikashindwa kupanda..ikaanza kurudi nyuma.
3. Bajaji ikawa unarudi nyuma kwa Kasi ikielekea Upande wa korongo.
4. Mm nikaona isiwe tabu maana nilikua nasikia harudlfu ya kifo.
5. Nikaruka, bhana wee
 
Haina fomula, ni sawa na kubeti tu. Kuna muda anayeruka anapona, wanaobaki wanakufa. Na kuna muda pia anayeruka anakufa, wanaobaki wanapona. Cha msingi ni kuangalia mazingira.
 
Mimi kilinikuta HV.
1. Tulikua kwenye bajaji tunaelekea huko mashambani..tulikua abiria watatu..mm nilikua nmekaa upande wa kushoto au mlangoni huku kwa abiria( kwa wanaopandaga bajaji watakua wameelewa)
Daaah, noma sana mkuu.
 
Nilikausha tu alafu ulikua mlima nyuma korongo derava kapanda na mbili ikaishiwa nguvu akabadili katikati ya mlima weehh uzuri aliekungia ktk kigema chabpembeni.
 
2. Tukafika kwenye kimlima fulani hv..Dereva akakomaaa weee mwisho bajaji ikashindwa kupanda..ikaanza kurudi nyuma.
3. Bajaji ikawa unarudi nyuma kwa Kasi ikielekea Upande wa korongo.
Haloo, hii kiboko...
 
Back
Top Bottom