DOKEZO Upigaji mradi wa maji Miwale Pangani Kibaha mkoa wa Pwani

DOKEZO Upigaji mradi wa maji Miwale Pangani Kibaha mkoa wa Pwani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JimmyKB

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
413
Reaction score
564
Habari wana JF? Niende moja kwa moja kwenye mada.

Kumekuwa na upigaji katika mradi wa maji mtaa wa Miwale kata ya Pangani wilaya ya Kibaha Mjini mkoa wa Pwani ambapo miaka kama minne iliyopita kulifanyika mradi wa maji uliogharimu milioni miatano lakini mradi huo ulikufa pasipo wananchi wa kijiji hicho kunufaika.

Hivi karibuni kumekuwa na mradi mwingine mpya kutoka DAWASA cha kushangaza mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Miwale amekuwa kikwazo kwa kutofuatilia mradi huo kwa manufaa ya jamii yake na badala yake amevuta bomba nyumbani kwake na kuwageuza wananchi wake mradi na kujinufaisha yeye binafsi kwa kuwauzia wananchi wake ndoo ya lita 20 kwa shilingi za kitanzania 100/= yakitoka bombani na shilingi 200/= yakiwa yamekwisha kujifadhiwa kwenye tanki.

Tofauti na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vikawe ambapo wananchi wake wameendelea kunufaika na mradi huo wa maji. Mwananchi mmoja mmoja mwenye uwezo amekuwa akitoa kati ya milioni 2 au zaidi ili kuunganishiwa maji hayo kutoka DAWASA huku wengine wengi wakijiunga kwa pamoja na kupeleka fomu zao za maombi ya kuunganishiwa maji ofisi husika.

Wananchi wa mtaa wa Miwale wanaomba viongozi wa juu wanao husika kulichunguza jambo hili na kulichukulia hatua zinazostahili ili waweze kupata huduma hii muhimu katika maisha ya mwanadamu.

Bila shaka ujumbe utawafikia walengwa wanao husika kwani Jamii Forum ni jukwaa lenye wigo mpana.

Nawasilisha ahsante
 
Back
Top Bottom