Upigaji PICHA kwenye maeneo ya wazi

Upigaji PICHA kwenye maeneo ya wazi

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,273
Reaction score
13,567
Wadau wa sheria naomba mnisaidie katika hili:

Sheria inasemaje kuhusu kupiga picha kwenye maeneo ya wazi (public).?

Miezi michache iliyopita nilienda kijiji fulani,na kubahatika kuhudhuria mkutano wa hadhara wa kijiji,bahati nzuri nikavutiwa sana na speech za wananchi,nikajikuta nachukua kamera yangu mfukoni na kuanza kuchukua video fupi"clips" ghafla wananchi wakaanza kunigombeza kwa maneneo makali kwamba siruhusiwi kuchukua video kwenye mkutano wao,au nijitambilishe kama mimi ni mwandishi wa habari wa serikali au la.?

Baadaye niliwaomba radhi na mkutano akaendelea bila mimi kuchukua video tena.Japokuwa ni kweli sikuomba ruhusa ya kupiga picha/video mwanzoni,je kuna kosa lolote nilifanya kisheria au wao kunizuia kuchukua video walifanya kosa.??

Nitashukuru kupata msaada wa kisheria.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom