HOJA Upimaji wa uzito wa nyama mabuchani unanipa mashaka kila siku

HOJA Upimaji wa uzito wa nyama mabuchani unanipa mashaka kila siku

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
KILO MOJA YA NYAMA INAWEZA KUWA KILO MOJA KWENYE MIZANI, LAKINI SIYO KWENYE UZITO HALISI?

Kuna jambo nimeanza kulifikiria sana kuhusu biashara ya nyama jijini Dar es Salaam.

Sijafanya utafiti rasmi, na sina ushahidi wa kumtuhumu mfanyabiashara yeyote. Lakini kama mlaji, nimeanza kujiuliza swali ambalo naamini linahitaji majibu kutoka kwa mamlaka husika.

Kwa muda sasa, nimekuwa nikiona kwamba ujazo wa nyama ninayopewa kama kilo moja unaonekana kuwa mdogo ukilinganisha na nilivyozoea zamani.

Hapo ndipo swali linapoanzia:

Je, kweli kilo moja bado ni kilo moja?

Au kuna uwezekano kwamba baadhi ya mizani zinazotumika kwenye butcheries hazitoi vipimo sahihi?

Kwa mfano, kama mizani imeharibika, haijafanyiwa calibration/verification ipasavyo, au imechezewa kwa namna yoyote, inaweza kumfanya mlaji aamini kwamba amenunua 1 kg, wakati uzito halisi ni chini ya hapo.

Na tatizo kubwa ni kwamba mlaji wa kawaida hana namna rahisi ya kujua.

Hatuendi butcher na mizani yetu. Tunaona namba kwenye display, 1.00 kg, tunaamini.

Ndiyo maana nadhani hili halipaswi kuishia kwenye “nahisi nyama imepungua.”

Nashauri mamlaka zinazohusika na vipimo na ulinzi wa mlaji zifanye ukaguzi wa kushtukiza katika butcheries mbalimbali Dar es Salaam.

Ichukuliwe mizani ya mamlaka, ipimwe dhidi ya mizani inayotumiwa na mfanyabiashara, na ikiwezekana zoezi lifanyike kwa maeneo tofauti, hasa maeneo yenye biashara kubwa ya nyama.

Kama mizani ziko sahihi, tutaondoa mashaka.

Kama kuna mizani zisizo sahihi, tutakuwa tumegundua tatizo linaloweza kuwaathiri maelfu ya walaji.

Na kama kuna mtu anachezea vipimo kwa makusudi, basi hilo si suala la biashara tu, ni suala la kuwaibia walaji kwa kutumia vipimo visivyo sahihi.

Kilo moja inapaswa kuwa kilo moja. Si 1.00 kg kwenye screen tu, bali 1.00 kg kwenye uzito halisi.

Mamlaka, tunaomba verification.

Hili ni swali la mlaji na wito wa uchunguzi, si tuhuma dhidi ya butcheries zote au wafanyabiashara wote.
 
Anaefanya hivyo ana lakujibu mbele ya Mola wake, kwa sasa ataendelea hivyo bila khofu yoyote, atakula bata wee, wala hawafikirii ipo siku wataondoka, je utaondoka na matendo gani!!! Allah atujaalie mwisho mwema
 
Bora mizani nyama unapewa unaiona. Sheli unawekewa mafuta huyaoni wala hujui yanaingia kiasi gani we unaamini tu kwamba umewekewa ya afu thelasini. 😐
 
Bucha nyingi ni wezi wakubwa hilo halina pingamizi na mamlaka za vipimo zimelala sana tunachakazwa sana nyama kilo ni km robo tatu tu.
 
Back
Top Bottom