Upinzani anzeni kuibua hoja na sera mbadala za kulikomboa taifa, acha kudandia na kuongelea upuuzi wa wana CCM

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,730
Reaction score
2,230
Hivi upinzani umeishiwa kabisa hoja na sera za kuwasemea wananchi na taifa letu kwa ujumla mpaka wadandie mabaya na matusi ya wana CCM?

Tunafaidika nini sisi wananchi kwa kutukanana wana CCM? Taifa letu litapataje maendeleo kwa kujadili matusi wanayotukanana wana CCM?

Kwani kuna jipya lipi alilolisema Paul Makonda kuhusu kuzodoana kwa wana CCM?

Hatukumbuki Kikwete alivyosema wana CCM hawaachiani maji ya kunywa?

Hatukumbuki sumu aliyowekewa Mwakyembe na wana CCM wenzake?

Hatukumbuki jinsi Phillip Mangula alivyoponea chupuchupu kufa kwa kuwekewa sumu alipokuwa kwenye kikao cha CCM?

Hatukumbuki matusi ya Kinana, Nape na Makamba kwa Hayati Magufuli?

Hatukumbuki Rais Samia alivyosema watakaomsumbua ni walioko ndani ya CCM na si upinzani? Kipya kipi?

Inasikitisha mno kwa upinzani kuishiwa kabisa hoja na sera za kutukomboa wananchi.
 
Hakuna upinzani bali kuna wapiga vinanda tu

Huwezi kusikia wakishika dola watafanya nini?

Hawawezi kunishawishi kitu hao

Kila mmoja anaangalia familia yake watakula nini na sio maendeleo yetu
 
Lini mtoa hoja utaanza push back yako bila ya kutegemea upiganiwe kupata haki zako?why utegemee mtu mwingine akupiganie?

Elewa kwako na familia yako maisha yaliendelea vema wakati Mbowe aliwekwa jela more than 200 day's, hakunyosha kidole chako kuuliza au kuingia mitaani,ulitulia kimya huku familia na wapendwa wa Mr.Mbowe wakihangaika wenyewe,stand up na pigana mwenyewe
 
Hivi upinzani umeishiwa kabisa hoja na sera za kuwasemea wananchi na taifa letu kwa ujumla mpaka wadandie mabaya na matusi ya wana CCM...
Gwapo, nikwambie tu kuwa hakuna uponzani nchi hii ukiwa kitaasisi,upinzani wa nchi hii ni mtu mmojammjoa na hivyo huongea kama kuku aliekatwa kichwa, yote kwa yote karibu CCM, halafu vipi uchambuzi DW, Mzee Mohd abdulrahman yuko wapi?
 
Sidhani kama watakusikia. Maana wapinzani wetu kwa miaka nenda sasa wanaendesha siasa za matukio na pia wengi wao ni wachumia tumbo. Yaani kwao siasa ni ajira!

Na pia hawajikiti katika kutengeneza sera mbadala na zenye mashiko, za kuikomboa nchi kutoka kwa watawala wa CCM.
Umenena vema sana
 
Lini mtoa hoja utaanza push back yako bila ya kutegemea upiganiwe kupata haki zako?why utegemee mtu mwingine akupiganie?

Elewa kwako na familia yako maisha yaliendelea vema wakati Mbowe aliwekwa jela more than 200 day's, hakunyosha kidole chako kuuliza au kuingia mitaani,ulitulia kimya huku familia na wapendwa wa Mr.Mbowe wakihangaika wenyewe,stand up na pigana mwenyewe
Daima niko mstari wa mbele kujipigania na kusaidia kupigania wengine
 
Gwapo, nikwambie tu kuwa hakuna uponzani nchi hii ukiwa kitaasisi,upinzani wa nchi hii ni mtu mmojammjoa na hivyo huongea kama kuku aliekatwa kichwa, yote kwa yote karibu CCM, halafu vipi uchambuzi DW, Mzee Mohd abdulrahman yuko wapi?
Nimekupata sana! Bado nasikika DW, hususan kipindi cha maoni meza ya duara. Abdulrahman alishastaafu, ila anasikika mara mojamoja.
 
Hivi upinzani umeishiwa kabisa hoja na sera za kuwasemea wananchi na taifa letu kwa ujumla mpaka wadandie mabaya na matusi ya wana CCM?

Tunafaidika nini sisi wananchi kwa kutukanana wana CCM? Taifa letu litapataje maendeleo kwa kujadili matusi wanayotukanana wana CCM?

Kwani kuna jipya lipi alilolisema Paul Makonda kuhusu kuzodoana kwa wana CCM?

Hatukumbuki Kikwete alivyosema wana CCM hawaachiani maji ya kunywa?

Hatukumbuki sumu aliyowekewa Mwakyembe na wana CCM wenzake?

Hatukumbuki jinsi Phillip Mangula alivyoponea chupuchupu kufa kwa kuwekewa sumu alipokuwa kwenye kikao cha CCM?

Hatukumbuki matusi ya Kinana, Nape na Makamba kwa Hayati Magufuli?

Hatukumbuki Rais Samia alivyosema watakaomsumbua ni walioko ndani ya CCM na si upinzani? Kipya kipi?

Inasikitisha mno kwa upinzani kuishiwa kabisa hoja na sera za kutukomboa wananchi.
Wakianza hayo mahitaji yako utawaunga mkono au ndiyo mabezo tu?
 
CHADEMA ya sasa ni kama 'upinde' tu. ..
Ni Lema yule tunae mjua . Kalainikaa .kalegea ka shoga.
Pumbavuu
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Back
Top Bottom