Uchaguzi 2020 Upinzani bado sana kuiangusha CCM, Magufuli atashinda kiurahisi sana

Uchaguzi 2020 Upinzani bado sana kuiangusha CCM, Magufuli atashinda kiurahisi sana

Naunga mkono hoja, kwa Tanzania, upinzani wa kweli, a serious opposition ya kuing'oa CCM madarakani, bado sana!. Ukijumlisha na mafanikio ya miaka mitano ya Magufuli, kiukweli kabisa tarehe 28 ni Magufuli Mitano Tena!.
Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...
P
we subiri teuzi, maadam umeshaonekana kule Kawe plus kabila linakubeba kuwa na uhakika mkuu
 
Kwahiyo umefikia hitimisho kwa maono tu ya bibi yako ambaye ana IQ ndogo kuliko hata ya hao wajukuu zake wanaosoma elimu bure.
 
sasa kama kafanya maendeleo makubwa hivyo kwamba wewe na bibi yako mtampigia kura (atashinda), ni kwann anawahofia sana upinzani...yaani hadi kwenye media anataka aoneshwe yeye tu.

aweke uwanja sawa wa ushindani ndio mtapata kipimo sahihi cha kukubalika na watz wote
Uwanja upi huo uwekwe sawa ndugu yangu?

Mbona barua mnazo zote Amsterdam ameaandika weee mpaka kachoka sasa anatweet, watu wanapanda jukwaani wanaropoka kadri wanavyojisikia.

Lakini ukweli ni kwamba CCM imejiimarisha sana huu ndio ukweli mchungu na watu hawataki kuusikia.

Tarehe 28/10/2020 mapema watu watakuwa wamesharejea Brussels wanakunywa juice wewe umebakia flyover ya ubungo.

Mwisho na kwa umuhimu fanya kazi hakuna mtu atakuletea chakula mezani.
 
Niko Moshi kaka! Acha kudanganya watu.
Watu wanaonewa tu na kuvamiwa waunge mkono ccm.Yapo baadhi ya majimbo ccm ina nguvu lkn sio kihivyo.

Naondoka Mwanga nitakuwa Machame/Umbwe kama saa 5.00 asubuhi Jumamosi.

Nitakutafuta angalia inbox namba ya simu.
 
Wakuu habari zenu,

Nimeangalia hali ya kampeni inavyokwenda na nikasema ni vyema nilete machache niliyopata kujionea.

1. Upinzani unategemea umaarufu na uwezo wa mtu binafsi na sio kujiimarisha kitaasisi hivyo kujikuta hawana agenda zenye muelekeo wa kuleta maendeleo kwa Taifa na kubakia kupinga na kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali na wakati mwingine huwa wanaokoteza wagombea hadi ngazi ya Uraisi ni AIBU.

2. Katika Dunia ya sasa ambayo kila Taifa lipo huru katika kujitawala, wapinzani wanaamini mataifa ya nje ndiyo yatakayowaletea maendeleo na kuwapigia kura za ushindi wanasahau wenzao CCM wamejiimarisha hadi vijijini.

{Mwaka jana nilienda Bukoba kuwasalimia ndugu na jamaa, walifurahi sana kuniona maana ulikuwa ni muda mrefu tokea nimeonana na ndugu na jamaa zangu. Kitu kilichonifanya nifurahi ni maongezi kati yangu na Bibi yangu kuhusu uchaguzi wa 2020-2025 kwakweli Bibi aliniambia uchaguzi huu atamchagua Magufuli kwasababu amepelekewa umeme hadi Kijijini na pia alimsifu kupambana na mafisadi (nilimuuliza kivipi vita na mafisadi imemsaidia,jibu alilonipa akaniambia wajukuu zake wanasoma bure hayo kwake ni mafanikio na pesa zingine zinajenga Barabara ). Mwisho alinisihi na mimi nipigie kura CCM 2020-2025.}

3. Kazi alizozifanya JPM zinajieleza zenyewe yaweza kuwa yanaitwa maendeleo ya vitu lakini tujiulize yafuatayo:-

i/ Ukuta wa Mererani
Tumekuwa tunalalamika madini ya Tanzanite yanatoroshwa na kuuza nchi jirani lakini kwasasa ujenzi wa ukuta huu umeyalinda madini yetu na serikali kupata mapato.

ii/ Ujenzi wa miundo mbinu
Kwasasa tukubaliane sehemu kubwa ya nchi imeunganishwa na barabara za lami zamani kwenda mikoa ya kusini (Lindi na Mtwara) ilikuwa ni kama adhabu ila kwa sasa kama una private car Lindi masaa manne hadi matano unafika kutokea Dar.

Hii pia imechochea kukua kwa biashara kwasababu mzigo husafirishwa na kufika kwa wakati hivyo kufanya mahitaji muhimu ya kibinadamu kupatikana nchi nzima.

iii/ Mikopo Elimu ya juu
Serikali ya awamu ya tano imejitahidi katika kutoa mikopo kwa vijana wa elimu ya juu hasa wanaotoka katika familia maskini ili kuweza kuwasaidia vijana wetu kusoma na hivyo Taifa kutngeneza wataalamu ambao watalitumikia Taifa kwa kuajiriwa katika utumishi wa umma,kuajiriwa na wawekezaji au kuajiri na kutengeneza ajira kwa vijana wengine.

iv/ Umeme vijijini
Kwakweli kama utabisha hapa nenda kamuangalie youtube Bwana Bwege wakati akichangia mchango wake bungeni aliisifu serikali katika kusambaza umeme vijijini. Sote tunaelewa umuhimu wa umeme katika maisha yetu kwa hili tuu JPM anatakiwa apongezwe kwa kupewa miaka mitano mwingine.

v/ Mapambano dhidi ya Covid 19
Hapa alicheza kama Pele wakati mataifa mengine yakiwapiga raia wao wakae ndani sisi Watanzania tulikuwa kama vile hakuna linaloendelea na kazi ziliendelea kufanyika, kwakweli kwa hili wala hakuna ubishi msimamo wake ulileta mafanikio makubwa, tusipolisema hili leo bhasi hata miti itasema anastahili pongezi na maono haya unahitajika 2020-2025.

Yapo mengi sana aliyoyafanya JPM katika kipindi cha miaka mitano kiasi itachukua muda mrefu kuelezea kama:-
a. Ujenzi wa vituo vya afya
b. Ndege
c. Stiglers gorge
d. Standard gauge e.t.c

Maendeleo yanahitaji watu kuchapa kazi kwa bidii hakuna mtu atakayekuletea chakula mezani tunapaswa kupambana kwa kufanya kazi kwa bidii kama ni kilimo tulime kwa bidii na kama ni biashara basi tuzidishe ubunifu kupata masoko, maofisini tuongeze ufanisi tukifanya hivyo tutasonga mbele.

Magufuli 2020-2025 ataenda kufanya makubwa zaidi ni muhimu vijana tukampa support ya kutosha ninaimani atatatuvusha kuelekea kule tunapopatarajia (maisha bora).

Tarehe 28/10/2020 kura zote kwa JPM.

Tanzania itajengwa na Watanzania tuwakatae wazandiki na wafitini.

Viva JPM

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kwa jinsi Jiwe alivyowatukana wana Kagera, hakuna mhaya anayeweza mpa kura hata kwa utani, ndiyo mana walimzomea. Bibi yako kama ni kweli aliyasema hayo basi atakuwa na tatizo la msingi kama wewe au ndiyo sababu uko kama ulivyo.
 
Kwa jinsi Jiwe alivyowatukana wana Kagera, hakuna mhaya anayeweza mpa kura hata kwa utani, ndiyo mana walimzomea. Bibi yaki kama ni kweli aliyasema hayo basi atakuwa na tatizo la msingi kama wewe au ndiyo sababu uko kama ulivyo.
Hauwajui wahaya wewe unasimuliwa tuu, subiria tarehe 28/10/2020 uone kama hawatamchagua JPM nani asiyetaka maendeleo akachague watu wa kususa susa bungeni ?
 
Hizi ni zile post za kuandikiwa hapo Lumumba ..zinakuwa ndefu halafu mode of writing haibadiliki
Kwa hiyo unafikiri ushindi mtaupata maeneo gani kwa mfano hapa tanzania, ambayo mnafikiri mtashinda?
 
Hauwajui wahaya wewe unasimuliwa tuu, subiria tarehe 28/10/2020 uone kama hawatamchagua JPM nani asiyetaka maendeleo akachague watu wa kususa susa bungeni ?
Yani nisimuliwe kuhusu wahaya?
Nasema kura zikihesabiwa kwa haki Jiwe hata 30% hapati. Kuwa mkweli kundi gani katika jamii (Wanafunzi,Wakulima, Wafanyakazi,Wafanyabiashara)wanaweza kumpa kura jiwe? Naomba usikimbie swali
 
Hayo mengine pia umeambiwa na bibi yako au ni kwa akili zako mwenyewe? Ok si vibaya kama umepata chochote kitu.
1600023575-picsay.jpg
 
Subiri watakuja kukujibu, kwa sasa bado wako busy ku edit picha za 2015.
 
Back
Top Bottom