Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Nawasalimu wana JF, Poleni na Majukumu.
Baada ya salamu naomba niwasilishe uchambuzi wangu mfupi kwenu juu ya vuguvugu la siasa linaloendelea kwa sasa wakati tunapoelekea Oktoba 28, Nitagusia siasa za upinzani, Kupitia andiko hili lazima nikiri kuwa Upinzani ni kichocheo cha maendeleo hapa nchini kwahiyo upinzani unao umuhimu wake lakini upinzani huohuo haujitambui na pengine haujui wajibu wake kwa Watanzania na maendeleo yake kama inavyotakiwa, Pengine kwa nini nasema hivi ni kwa sababu upinzani unaishi kwa siasa za “Matukio” badala ya mipango na mikakati yenye agenda ya kushika dola.
Mathalani kwa kipindi hiki ambacho tunaona wagombea wa vyama vikuu vya upinzani kama ACT-Wazalendo na CHADEMA wanazunguka mikoani kutafuta wadhamini badala ya kujenga hoja za kiagenda kwa wapiga kura wao wanaibuka na hoja za kumshambulia mtu badala ya kujenga hoja, Upinzani jengeni hoja tuwasikilize acheni kumshambulia JPM na Dk Mwinyi tunahitaji kusikia sera zenu na si siasa za kushambulia washindani wenu, Aidha mtindo wa kupima ushindi wa kushika dola na “Mafuriko ya watu” Si mtaji kisiasa bali ni uchovu wa kifikra, uwezi kupima uwezo wa kushika dola kwa wingi wa watu ambao wengi wao si wapiga kura ni wahuni na wapambe nuksi.
Napenda kushauri upinzani kujikita kwenye ujengaji wa hoja zenye agenda inayoeleweka kwa wapiga kura na si kuanza kutangaza ushindi kabla ya wakati kwa sababu ya wingi wa watu wanaojitokeza kwenye mapokezi ya vyama vyenu, Tanzania tunahitaji upinzani unaojielewa kifalsafa na wenye agenda ya kutuvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kimaendeleo. Kwa mantiki ya kinachoonekana sasa ni vigumu kwa vyama vya upinzani kushika dola kwa sababu hawajajipanga kupambana vilivyo na chama tawala zaidi ya kujipanga na matukio yasiyokuwa na faida kwao kisiasa.