Uchaguzi 2020 Upinzani hawako serious kabisa kuiongoza nchi, sijui ni uvivu ama la

Uchaguzi 2020 Upinzani hawako serious kabisa kuiongoza nchi, sijui ni uvivu ama la

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
Habarini

Katika kutafakari tutafikaje 28 october, likanijia hili wazo tena fikra za kuanzia at family level

Kwenye familia, vikao vya kifamilia vikikaa yule mwenye uafadhali kimaisha ndie mara nyingi anakuwa anasikilizwa na kupewa majukumu ya kiuongozi the same as katika ukoo

Kwenye ubunge, mimi leo hii nikisimama na Abood pale Moro Mjini nina uhakika hata niteme cheche zinazounguza kama moto wa jehanamu sidhani kama wananchi watanielewa..! Zaidi zaid wataniita mchumia tumbo! Wenye nacho ndio huongezewa na kupewa zaidi

Kulingana na hayo mawazo nikaja kulinganisha na vyama vyetu hapa nchini... Tukianza tangu mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi uanze ni chama kimoja tu ndo kinashikilia hatamu. Nilipojiuliza kwani upinzani hawawezi?

Nikahusianisha na mifano ya hapo juu na kukichukua chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kama mfano tokea uhuru mpaka leo hawana jengo lao kama makao makuu bali wamepanga tu.. Na hakuna hata mradi wao mmoja tu unaofahamika!

Je, ukiwapa nchi si ndo watageuka kuwa wachumia tumbo?

NI HAYO
 
Wanaojua miradi binafsi ya vyama vya upinzani wanitajie
 
Aisee,kumbe 2015 alipaswa kuwa Lowassa na si Magufuli kwa mfano wako wa Aboud!
Hivi lumumba mmebakiza akil tu za kuvukia barabara?
 
Vyama vya siasa siyo makampuni ya biashara wewe zwazwa mpaka viwe na miradi.

Wewe guruguja taja mradi hata mmoja wa CCM ambao umejengea baada ya mwaka 95.
Dogo mbona una kichwa cheupe sana? hv unajua maana ya taasisi? kwanini chadema inajiita taasisi? kwa kukosa hata jambo moja ambalo wamelisimamia likaleta tija kwa wananchi au hata viongozi wenyewe basi hawafai kukabidhiwa nchi...

Mtu unashindwa hata kujenga nyumba yako miaka nenda miaka rudi afu unataka tukuamini kuwa utaweza kusimamia miradi yetu ya kimaendeleo?

Ukiwa na akili hata kidogo utaelewa lakini kama ni zile za kuungaunga na gundi ya mate basi nitajipa pole kwa kuvisulubu vidole vyangu kukuelewesha we kichwa maji
 
Aisee,kumbe 2015 alipaswa kuwa Lowassa na si Magufuli kwa mfano wako wa Aboud!
Hivi lumumba mmebakiza akil tu za kuvukia barabara?
tatizo alikosa sifa ndani ya chama, na laiti kama chama kingempitisha, basi ye ndo angekuwa rais wa tanzania hv sasa... ubaya ni kuwa kaenda chama kilekile ambacho kinashindwa kujitegemea na kuamua kuishi kwenye nyumba za kupanga
 
tatizo alikosa sifa ndani ya chama, na laiti kama chama kingempitisha, basi ye ndo angekuwa rais wa tanzania hv sasa... ubaya ni kuwa kaenda chama kilekile ambacho kinashindwa kujitegemea na kuamua kuishi kwenye nyumba za kupanga
Kama kuwa CCM ni kushinda,mbona kuna wabunge wapinzani wengi tu?Mbona Maalim Seif alishinda 2015 ila mkaunajisi uchaguzi na kuufuta?
 
Wewe acha kuongea usivyovielewa! Chama cha siasa mtaji wake ni siasa safi na sera zenye kugusa mahitaji ya wananchi na wala sio utajiri au uwingi wa miradi! Kwanza hata hao matajiri tuliowaingiza kwenye siasa ilikuwa ni makosa ila tu wamefumbiwa macho kwa vile mnufaika ni chama kilichoko ikulu!

Mbunge hapaswi kuwa mbunge na hapohapo akawa mfanya biashara, Huyu bungeni hawezi kupitisha sheria zitakazomnyima faida ya biashara zake! Pia hata icho chama chako unachojaribu kukinadi kwa miradi hakina lolote la kujinia na miradi hiyo maana kwenye chaguzi karibu zote zilizopita tumekuwa tukisikia mtu kaingizwa ikulu baada ya mabilioni ya fedha za serikali kuchotwa.

Mfano mwaka 2005, kuna mabilioni ya senti zilichotwa toka account ya EPA, mwaka 2015 napo kuna mabilioni ya vijisent yalichotwa NSSF ndipo Mgombea wenu akaingia ikulu! Mwaka huu nao tutasikia tu muda si mrefu maana kuna Trion 1.5 ambazo mpaka leo hazijulikani zilipo na wala matumizi yake hayajawahi kuwekwa bayana!
 
Back
Top Bottom