Uchaguzi 2020 Upinzani hizi dakika za majeruhi naona Dkt. Magufuli anatuumiza sana na hoja ya korona, tujipange kumjibu

Anatuumizaje sasa, magufuli alizuia kuendelea kuchukuliwa kwa vipimo vya corona, kama ana guts aruhusu vipimo viendelee kuchukulia.

Ujinga wake zaidi ulikuwa kutuma ndege na kabudi mimacho kwenda madagascar kufuata dawa za ugonjwa mnaojitapa tapa kwamba haupo.
 
Lissuuu jomba Ni mkombozi wa mambo gani muwe mnatuambia nasisi tujue...kizuri kula na mwenzako jomba..msiwe wachoyo
 
Hata Magu anavyosema maendeleo hayana chama huwa ni siasa tu na ndio maana sasa hivi anataka achaguliwe wabunge na madiwani wa ccm ndio ili apeleke maendeleo sehemu husika.
Jomba unajua maana ya slogan ya maendeleo hayana chama..?? It means hata ikijengwa hospital, watakaotumia hawabaguliwi kichama, cuf, act, chadema, nccr, CCM, tadea na wengineo woote watapewa huduma pale..ongeza na mifano mingine hapo, nenda madawa, Barabara, madaraja, ndege, meli, pantoon, sgr, etc
 
Jomba kwa mfano wewe unaweza tuambia Corona haijakupata mpaka leo umetumia Nini Kama kinga, au ndugu zako wameshakufa wangapi ukilinganisha na wale wanaokufa na kuambukizwa ulaya kila siku..tuambie Ni miujiza gani Tanzania imetokea mpaka hata kampeni zimeendeshwa hivi...Marekani waliandamana tu kwa wiki moja wakakuta maambukizi ya watu zaidi ya 50,000..tuambie Siri iliyo nyuma ya pazia kwa nchi yetu ili tuelewe..pls tell us, msituambie maneno ya hovyohovyo Kama watu waliorukwa na akili..
 
Wafanya biashara mliozoea kuwa mnakwepa Kodi, wizi, madili, utapeli tunaelewa machungu mlionayo Sana..inabidi mumsamehe JPM, maana Hana jinsi..anataka kujenga nchi lakini kwa mapato ya ndani.mapato .yatatoka wapi Sasa Kama sio Mimi na wewe...hatuwez Rudi nyuma kwenye ile enzi ya maisha ya utapeli..ukweli mchungu huu..vumilieni anzisheni kazi halali na mzoee kulipa Kodi..acheni ujinga..maisha ya utapeli mnayoishi mtakuja umbuka..nendeni hata mkapime zabibu dodoma..hayayote uliyoyaandoka ni matokeo ya kuminywa kwa mabiashara yenu ya utapeli na ukwepaji kodi
 
Tulishafanya maamuzi mambo ya Corona siyo habari mpya ni kama Ukimwi tu na Malaria...
Mlifanya maamuzi lini jomba..mara ya mwisho tuliwaona mmevaa barakoa mkatoka bungeni eti mtaambukizwa..so mlienda kuji caranteen. Right?.. Sasa tangu mlivyorudi bungeni hamkutuambia Kama Corona ilishaisha au kulitokea Nini..au mlipata dawa . Mlipiga kimya mpaka leo. Hamjatuambia lolote.sasa hayo maamuzi mliyafanya mkiwa wapi..jomba..hatutaki uongo..kuweni wakweli..msidhani watanzania hawa hawana akili Wala hawaoni..subirini adhabu yenu tarehe 28..tumewachoka
 
Hoja zipi?
 
Alikimbia korona akajificha miezi 3,sisi si kisiwa chukua taadhari Siri ya corona tafuta madaktari uwaulize
Ukaulize daktari wakati mtaa wenu una makaburi na majirani na ndugu unao? Nafikir hayo ndio inhekuwa kipimo kwamba kule makaburini kuna ongezeko la kiasi gani? Je ndugu wamekufa wangapi? Majirani je? Mfanyakazi mwenzio je?
Na hayo unaweza kufanya utafiti kwa kutumia akili zako tu na siyo lazima Lisu aje akwambia.
 
Lazima awapige kisawa sawa
 
Mambo serious ya nchi na wapo watu wamekufa, wazalendo wamekufa unasema apotezee kirahisirahisi hivyo. Wewe kwa sababu hujapata msiba wa Corona. Ndio maana..acha ujinga..unajua jinsi ambavyo nchi nyingine zinavyosota na hili gonjwa...hatudanganyiki jomba.mpaka mshike adabu za mama zenu
 
Corona aliiondoa Mungu kwa kupitia jitihada gani jomba au unadhani Mungu anachukua hatua na maamuzi Yeye mwenyewe bila wewe kuonyesha jitihada..hahaha hivi una akili wewe ya imani..usimchukulie poa Mungu wetu..Ni lazima unyenyekee na kuomba..kutwa kucha mnatunga uongo..Nani angewaponya na Hilo gonjwa...lazima uelewe kuna mwanamume wa shoka alisimama na kuongoza wananchi kwa kauli moja nakuwasilisha maombi kwa Mungu na Mungu akajibu maombi..mkae huko mkijua bila Magufuli saiz mngekuwa bado lockdown tangu wabunge wenu walivyokimbia bunge eti kaenda caranteen...pumbaa..afff kabisa
 

Yaani Magufuli atapata kura kwa kuongelea corona ugonjwa ambao haujatuathiri watanzania kwa kiwango hicho? Au mnataka kuhalisha huu wizi wa kura alioupanga? Kama amepambana na corona, mwambie apambane na magonjwa kama ukimwi, kisukari nk, kisha akayashinda uje ulete mrejesho. Kama nyie ni wajinga, msilazimishe kila mtu awe mjinga.
 

Hamna Mungu fala wa hivyo. Mama yake Magufuli yuko kitandani muda sasa, amuombee kwa huyo Mungu wake tuone ukweli. Huo ujinga waambieni wasiojua ukweli wa huo ugonjwa.
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
Jidanganye tuu,upinzani ungekuwa dhaifu msingetumia tume kuwakata wapinzani hivyo na pia ungekuwa dhaifu huyo Jiwe wenu asinge kuwa anatapatapa kujibu nondo za Lissu,kila kukicha eti anatangaza upuuzi
 
Mbona Lisu anakumbushia risasi wakati ni miaka kibao..Covid 19 mpaka sasa ni habari ngumu Duniani lakini huyu Magufuli alituongoza vyema kukabiliana nayo.


October 28th ni landslide victory kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Hamna Mungu fala wa hivyo. Mama yake Magufuli yuko kitandani muda sasa, amuombee kwa huyo Mungu wake tuone ukweli. Huo ujinga waambieni wasiojua ukweli wa huo ugonjwa.
Kwahiyo ukweli wa ugonjwa ukoje tuelezeni basi...mara ya mwisho mlikimbia bungeni mkaenda kuji caranteen mwisho wake mkarudi kukaa na wale wale mliowakimbia...mlikuwa mna maana gani. Hamjawahi kitoa statement yoyote tangu hapo..kimya kimya tukawaona mmeanza kuvua barakoa bila kuwaambia wananchi...Stu..ip.i.d..mnadhani wananchi hawajawaona...mnawafanya watanzania wajiiinga...hahaa
 
Usipochagua mbunge na diwani wa ccm hapeleki maendeleo eneo hilo,sasa hapo utasemaje habagui? Ingekuwa maendeleo hayana chama basi hata akiwepo mbunge wa Chauma bado atashirikiana nae kupeleka maendeleo kwa sababu maendeleo hayana chama.
 

Watu kibao tunajua ukimwi upo na wala hatuvai kondom. Kutofuata taratibu za kupambana na ugonjwa, hiyo haimaanishi huo ugonjwa umeisha. Mimi ni mwananchi na ninajua serikali wala maombi sio yaliyoondoa huo ugonjwa, bali huo ugonjwa haukuwa na madhara makubwa kwenye ukanda wetu. Mtanzania yoyote anayeamini serikali na maombi ndio yameondoa huo ugonjwa, ni mjinga kama mjinga yoyote. Imeisha hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…