Mabibi na mabwana heshima kwenu.
Tunapoendelea kusonga mbele na jitihada za kuleta mabadiliko ambayo kila aliye mzalendo angeyapenda, wenye mawazo mgando wanazidi kuingiwa mchecheto.
Hofu imewatanda hawakumbuki jana walisema nini, leo wasemeje wala kesho watasema je.
Palikuwa na hadithi, Lissu harudi. Mbowe hatamwachia Lissu kugombea urais. Lissu akirudi atakamatiwa JNIA. CHADEMA mgombea atakuwa Nyalandu. Lissu hatapata uteuzi wa tume.
Mara oh, Lissu atashikiliwa na mahakama kwa ajili ya kesi zake ambazo nazo ni za kubumba bumba tu nk, nk.
Yakawepo, Membe anakuja kuvuruga upinzani. Membe ni pandikizi lao yupo kwenye kazi maalum, nk, nk.
Ambayo hawakuyataka ndiyo yanakuwa. Wameshikwa pabaya wao na wapambe wao. Kote nchale. Wakisimama nchale, wakikakaa na hata wakichuchumaa nchale.
Wamepagawa na wanaweweseka. Kwa hakika wamechachawa hawajui washike wapi.
"Wenzangu mliwapa miaka kumi kumi mbona miye mnipe mitano tu?"
Aku! Kwani ni zawadi tu bila wajibu?
CHADEMA na ACT hongereni kwa kuzitambua zilizo kelele za vyura na kuzipuuza vilivyo. Mmethubutu Ila safari bado. Tungali tunasubiri ile ahadi yenu kuu:
"Msipokuwa na mgombea mmoja wa upinzani Watanzania hawatawaelewa."
Wako wapi NCCR na mzee wa SMS za usiku kwa Mzee baba? Haiyumkiniki angali anaendeleza libeneke lake!
Yuko wapi yule propesa libumba na CUF aliyoachiwa? Atavuna wabunge na madiwani wangapi Zanzibar 2020? Kusoma hujui hata picha kuangalia wajameni?
Yuko wapi Spunda na bwabwa lake na ndizi mbivu za kushushia? Pamoja na yote mkuu Spunda umetikisa Ila hawa wenye mawazo mgando. Tuwatoe kwanza, ubwabwa tutakula tu tukishamalizana nao.
Wako wapi hawa wengine ambao hata majina yao tu wapiga kura walio wengi hawayajui?
Tanzania ya leo inahitaji haki, uhuru na maendeleo au bata kama wengine wanavyoita. Maendeleo ya watu kabla ya maendeleo ya vitu. Haki na uhuru wetu haviwezi kuwekwa daraja la pili dhidi ya vitu.
Wanayo haki wenye mawazo mgando kuingiwa mchecheto.
Na bado!
Hadi sasa hawajatamka uhuru wala haki popote pale. Kwao wao uhuru na haki zetu si suala bali madege yasiyokuwa na cha kufanya na zaidi ya 95% ya watanzania.
Kwamba kwani hata ni miundo mbinu basi? Labda kama ni Dar, Dodoma na Chato. Kwa maana kwingine kupo hivi:
Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo
Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo
Wakati Chatto kupo hivi:
Chato kupo hivi. Je, hii ngozi haivutwi mno?
Ajisifuye, kwa miundo mbinu ipi?