Ndugu zangu wasalam,
Ukiangalia mambo yanavyoenda kasi nchini kwetu, huwezi amini wapo watu wanasuka mipango kila uchwao kuhakikisha vyeo vyao na maslahi yao hayaguswi, kuondoka kwa Magufuli kumeibua mengi ila moja ya mipango ni kama ifuatavyo;
Kwamba MATAGA wote wana mpango wa kuomba radhi wapinzani na kurudi kundini na kupush agenda zitakazomtikisa Rais Samia hadi asalim amri awarudishe kundini, na hii ya kuomba radhi imeanza kwa kasi, lakini agenda za kumtikisa Rais zaidi ni kama zifuatazo
1. Chadema na hasa upinzani waanze kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi sasa ivi ili mambo yaanze kuparanganyika na wao wapate vitoweo, huo mkakati hata huku JF unaweza uona toka kwa watu credible sana.
2. Kwamba Chadema na hasa upinzani washirikiane na vyama vya wafanyakazi kudai nyongeza ya mishahara, mazingira ya kaz na malipo ya Pension ikiwemo NSSF.
3. Kumtengenezea Rais Samia matukio na kuanza kuhamia upinzani, wale wale waliokuwa wanawatesa na kuwabambikia kesi
4. Mnec wa moja ya mikoa kanda ya ziwa ananiambia wimbi la wazalendo feki wanataka kuanza kutumia udini na Uzanzibari kama kete ya kutaka kumuondoa Rais kwenye track.
5. Kuna issue ya Muungano na serikali tatu itatumiwa sana na hilo kundi la 'wazalendo" kwa mgongo wa upinzani.
Niwambie tu wapinzani na hasa CHADEMA (So far ndio chama cha upinzani cha maana) muacheni Rais aiweke nchi vizuri kwanza bila distractions na bila hila za unafiki za watesi wenu, hao wanaomba msamaha kwa kujidai waungwna wameshaua na kuteka wanachama wenu wengi sana, jiulizeni tu kwanini sasa? uchaguzi wamewadhulum na matusi na vipigo juu, bado mje mkomae nao kwa msingi wa maridiano ni 'uhuni' wa kiwango cha juu sana, lakini pia tutawadharau sana.
Wasalaam,
Mirisho.