Upinzani ni fikra sio chama, haufi

Upinzani ni fikra sio chama, haufi

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kuna wanaofikiria vyama vya upinzani na fikra za upinzani ni kitu kimoja. Tanzania watu wana utamaduni na fikra za kupingana na ubishi hii hakuna mtu ataweza kuiondoa.

Ilikuwepo kabla ya uhuru mpaka sasa.
Vyama vitakufa kwasababu ni taasisi zinazoweza kubanwa lakini fikra ya upinzani ni kama dini iko ndani ya watu na kamwe haitakufa.

Upinzani wa fikra sio kupinga serikali lakini kama mtu binafsi ni kupinga chochote ambacho unafikiria hakiendi vizuri.

Hakuna hata Mtanzania mmoja ambaye finger print yake inafanana na mwingine. Mungu kaumba kila mtu tofauti na yule ambaye anajifanya kila kitu mko sawa na mawazo yako yote, fikra zako zote ana support kuwa naye makini sana.
 
Lakini aghalabu huwa kunatokea watu wawili au zaidi wenye kushabihana fikra, ndiyo sababu ya kuunda alliance.
 
Huwezi kutenganisha maendeleo/mafanikio ya taasisi na fikra. Fikra huzaa taasisi, taasisi hufa fikra zikifa! No need of stupid excuses, matokeo ya sasa ni zao la maamuzi yenu mwaka 2015 na kutotaka kuwajibika kwa failure zenu!

Simple fact!
 
Mtoa mada upo sawa, mawazo mbadala ni muhimu sana kwa ustawi wa taifa lolote, Muhimu ni kuwa na katiba bora yenye mifumo na taasisi imara. Mfano mashariti kwa chama cha siasa yangekuwa magumu ku filter vibakie vichache vyenye nguvu. Tunahitaji jifunza kitu BBI ya Kenya pia.
 
Back
Top Bottom