Uchaguzi 2020 Upinzani ni sera mbadala, si 'kuunga mkono juhudi'

Uchaguzi 2020 Upinzani ni sera mbadala, si 'kuunga mkono juhudi'

Ta Nanka

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
1,351
Reaction score
2,079
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaoelekeza mashambulizi kwa upinzani, hasa mgombea wa CHADEMA, T. A. Lissu. Katika mazingira ya uchaguzi ambapo chama kimoja kinaomba kura kurejea madarakani (chama tawala) na vyama vingine (vya upinzani) vinatafuta kukiondoa madarakani chama tawala, ni udhaifu mkubwa kwa wapenzi/wafuasi/wanachama wa chama tawala kutumia muda mwingi kueleza ni kwanini wapinzani hawafai kupewa madaraka.

Kinyume chake, wapinzani ndio hasa wanatakiwa kueleza kwanini waliopo (chama tawala) hawafai, ili wapewe wao. Hii ndio kazi hasa ya chama cha upinzani vinginevyo mwelekeo wowote wa “kuunga mkono juhudi” ni upuuzi tu. Chama cha upinzani kinapaswa kuwa na sera mbadala, (vinginevyo hakifai kuwepo) na kazi yake ni kueleza ni kwanini sera zao ni bora kuliko zilizopo (za chama tawala). Kwahiyo hapo ni lazima kueleza mapungufu ya sera zilizopo huku ukinadi zako. Kama kuna watu wanataka upinzani ufanye kazi ya kusifia chama tawala, hao hawajui hata maana ya kuwepo siasa za vyama vingi.

Kazi kubwa ya chama tawala kwenye uchaguzi ni kueleza kimefanya nini na kinatarajia kufanya nini. Haitarajiwi na ni aibu kwa chama tawala kuanza kufanya kazi ya kueleza ni kwanini wapinzani hawafai kupewa nchi. Kama kimefanya mazuri huo ndio mtaji wake. Sasa unapoona wimbi kubwa la wapenzi/wanachama wa chama tawala wakitumia muda mwingi kutueleza ni kwanini upinzani (au mgombea fulani wa upinzani) haufai kupewa nchi, mtu unabaki unashangaa. Yaani chama tawala kinaanza kujivika upinzani. Hii ni aibu!
 
CCM ni sawa na mtalaka ambaye bado anang'ang'ania ndoa ijapokuwa kesha pewa talaka tatu. Yaani wapigakura walisha fanya mambo yao ktk sanduku la kura toka 2015 kwa huku Bara, na 1995 kule Zanzibar, lkn bado wanalazimisha kupendwa tu.

Ebu makada kuweni basi waelewa hata kidogo jamani! Mavazi ya rangi ya kijani yameshatuchosha sana, wananchi wanataka yakawekwe kwenye jumba la makumbusho pamoja na mwenge wa uhuru, ili vizazi vijavyo vikapate kuona adui wao mkubwa wa maendeleo kwa miaka mingi iliyopita.
 
JamiiForums1323532925.jpg

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom