Hayo maandamano yanayoruhusiwa ndio police wanakuja kutandika risasi za moto, mbaya zaidi hadi Mungiki na wao wanavalishwa jezi za police kwenda kuua Jaluo, nyie ni jamii isiyo na huruma kabisa.
Ndio, Tz mikutano ya kisiasa inayoruhusiwa ni viongozi wa sehemu husika, kama wewe ni Mbunge wa Kajiado, fanya mkutano na wananchi wako wa Kajiado, hakuna haja ya kwenda kufanya uchochezi Nairobi. Huo si utaratibu mbaya na unaleta utulivu wa kisiasa.
Tz kuna sheria ya takwimu, mtu akionekana anafanya maksudi kupotosha takwimu ataenda kujielezea mahakamani, wao ndio watamuhukumu na takwimu zake za kupika. Kuruhusu wanasiasa waropoke uongo wowote kwa jina la uhuru si ushujaa, ni ujinga. Mwanasiasa anageuza takwimu kwa maksudi ili tu atengeneza chuki, hii si uhuru wala demokrasia, acha wakufundishwe adabu mahakamani.