Blackafrica
Senior Member
- Jun 26, 2021
- 141
- 401
Ukweli ni kwamba Watanzania wengi wamekichoka Chama cha Mapinduzi, lakini ni ukweli pia nje ya Chama cha Mapinduzi hakuna chama mbadala, kwa sasa upepo umebadilika, baada ya kifo cha Magufuli kuna kundi kubwa la wanyonge ambao kwa wingi wao walikuwa ni wafuasi wa mwenda zake, kwa sasa hili kundi limebaki yatima na kiukweli wanasubilia mwaka 2025 kuonesha hasira zao kwenye box la kura.
Kuna kundi lingine ambalo automatic hawakielewi Chama cha Mapinduzi na wanatamani upinzani uchukue nchi, fursa iliyopo hapa ni upinzani kumsimamisha mgombea ambaye atakuwa anakubalika na makundi yote, kuanzia kundi la wanyonge au wafuasi wa mwendazake na makundi mengine ya wanaharakati wa upinzani na wakereketwa wa upinzani, nina hakika safari hii ikulu mtaingia.
Mgombea ambaye upinzani wanapaswa kumsimamisha awe kigogo kutoka chama cha mapinduzi, hii ndio fursa adhimu ambayo upinzani wanayo, hata CCM wameshtuka ndio maana wana muhada mwenyekiti wa Chadema, kwa kumpa ahadi ya kumjumuisha kwenye serikari baada ya uchaguzi ili wasijiongeze kutafuta wagombea urais wenye nguvu, nataka kuwashauri upinzani mkiwapata watu kama profesa kabudi, Lukuvi, Majariwa, Ndugai ikulu mnaingia asubuhi na mapema msiwalete watu kama Membe ambao hawakubaliki na kundi la mwendazake. Nimetimiza wajibu wangu wa kushauri kazi kwenu.