Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Nchi zote hizo zina demokrasia iliyojengwa kupendezesha kundi fulani katika jamii. Marekani demokrasia yao iliandikwa kumlinda mzungu na mali zake kabla ya marekebisho ya hapa na pale. Wahindi wa asili wa Marekani hawawezi kupata nafasi ya juu ya kisiasa bila baraka za mzungu, Obama mwenyewe alizungukwa na wazungu ndio akaweza kutoboa, angenda mwenye na waswahili wenzake asinge fika hapo alipo. Uturuki ni hivyo hivyo, jamii ndogo kama hizo za wakurdish, haziwezi kuwa na sauti ya kisiasa bila kujingiza kwenye muungano na vyama vingine vikubwa kama AKP na HDP. Demokrasia ya kweli ni ile inayotowa nafasi za kila raia na sio baadhi ya watu. Ndio shida ambayo naona kwa mtu anayetoka Malindi kupewa nafasi ya kuongoza chama kama Jubilee. Demokrasia sio nafasi ya kusimama na kutoa maoni halafu wakati wa kushika usukani wanashika wengine wewe ukiwa msindikizaji tu.Kwani Merakani hawana ukabila? Uturuki hawana ukabila? Leo hivi ni vigumu sana mtu mwenye asili ya Latino kuchaguliwa rais na Obama alipata baada ya miaka 235 ya ubaguzi .Pale Uturuki vigumu sana mtu mwenye asili ya Kurdish kuwa rais wa Uturuki.